Afrika Kusini-Mashambulizi

Maduka ya wageni jijini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini yashambuliwa na kuporwa

zaidi ya Maduka 150 yanayomilikiwa na Raia wa Somalia yamevamiwa na bidhaa kuibiwa mjini Port elizabeth nchini Afrika kusini, Jeshi la nchini humo limeeleza.Vurumai hizo zilisababishwa na tukio la kifo cha kijana mmoja ambaye anadaiwa kuuawa na mmiliki wa duka ambaye ni Raia wa Somalia, baada ya kuzozana juu ya Muda wa maongezi wa simu ya mkononi.

Matangazo ya kibiashara

Tangu jumapili juma lililopita, matukio ya uvamizi na unyang'anyi dhidi maduka 150 ya Raia wa Somalia yalipamba moto na vurumai hizo kuenea katika miji mingine, Jeshi la Polisi limeeleza.

Mamlaka nchini Afrika kusini imesema Takriban watu 111 wamekamatwa wakihusishwa na vurugu hizo na watafikishwa mahakamani juma hili.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hali ngumu ya maisha kwa wazawa wa nchini humo na ukosefu wa ajira, imechochea kuwepo kwa ghasia za namna hiyo hasa dhidi ya wahamiaji.

Mashambulizi ya aina hiyo yameonekana kushika kazi na kutanda katika mikoa mingine ambapo wananchi wanasema wanalipiza kisase, huku katika maeneo mengine maduka yanayo milikiwa na wa China yameshambuliwa pia.

Hali bado ni tete katika mji wa townships huko Port Elizabeth ambapo polisi wamemiminika kwa wingi kuhakikisha usalama unadhibitiwa katika eneo hilo.
Askari polisi mmoja amejeruhiwa wakati wa urushianaji mawe na raia hao waliokuwa wakishambulia maduka ya wageni.

Machafuko ya aina hiyo yamekuwa yakushuhudiw amara kadhaa nchini humo ambapo mwaka 2008 watu zaidi ya elfu sitini walipoteza maisha wengi wao wakiwa ni wageni.
Kituo kinacho hudumia wahamiaji kimesema wageni 140 wamepoteza maisha mwaka uliopita, huku 250 wakijeruhiwa mwaka uliopita.

Mmoja kati ya wageni walioshambuliwa nchini humo Faisal Ahmed ambaye ni raia kutoka nchini Somalia, amesema wamekimbia vita nchini mwao na kukimbiulia nchini humo wakiwa na matumaini ya kueshi vizuri lakini inasikitisha kwa sasa wanachukuliwa kama wanyama wakati walitetegemea kuwa raia wa Afrika Kusini ni ndugu zao.