Nigeria-Mauaji

Watu 87 wauawa katika shambulio la kundi la Boko Haram nchini Nigeria

Takriban watu 87 wameuawa nchini Nigeria katika shambulio lililoendeshwa na wapiganaji waasi wa kundi la Boko Haram waliokuwa wamevalia sare za kijeshi katika mji uliko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, viongozi wa serikali wamethibitisha. Saidu Yakubu kiongozi mmoja jijini Borno amesema Miili 87 imeokotwa porini na wanajeshi wa serikali bado wanatafuta miili mingine. Gavana wa Mkoa huo Kashim Shettima ametembelea katika eneo la tukio kushuhudia mauaji hayo.

wapiganaji wa kundi la Boko Haram
wapiganaji wa kundi la Boko Haram
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashuhuda, Wapiganaji wa kiislam wa kundi hilo la Boko Haram wamteketeza pia kwa moto majumba kadha na kuwapiga risase wale wote waliojaribu kutoroka.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba tukio hilo limetokea siku jumatano katika mji wa Borno ambao umekuwa tishio kubwa mwa mashambulizi kutoka kundi hilo.

Mawasiliano ya simu katika mji huo yalikatika tangu katikati mwa mwezi Mei pale serikali ilipotanganza amri ya hatari katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo wakati ikiendesha operesheni ya kumaliz auasi wa kundi hilo la Boko Haram.

Hatuwa hiyo ya kukata mawasiliano ya simu ililenga kuwazuia wapiganaji hao kuratibu mashambulizi, hali ambayo imesababisha hata wananchi kushindwa kutowa taarifa za dharura, hasa pale wanaposhambuliwa na wapiganaji hao.

Kulingana na duru za kiusalama katika mkoa huo ambazo hazikupenda kutajwa, wapiganaji hao walikuwa katika malori zaidi ya ishirini wakiwa na silaha nzitonzito
Mallam Isa Manu muendesha pikipiki ambaye alifaulu kutoroka, amewaambia waandishi wa habari mjini Maiduguri kwamba waasi hao wa Boko Haram walikuwa wamevalia sare za kijeshi, ambapo sio mara ya kwanza wanatumia mfumo huo katika kutekeleza mauaji.

Kwa mujibu wa jenerali Mohammed Yusuf, wanajeshi walijikuta wakiishiwa uwezo wa vifaa wa kupambana na wapiganaji hao.

Hata hivyo shambulio hilo halikujulikana, Boko Haram imekuwa ikiendesha mashambulizi dhidi ya raia waliunda makundi ya vijana kwa ajili ya kujihami katika kuwasaidia wanajeshi kutekeleza operesheni yao.