Maandamano yazuka nchini Sudan baada ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta
Imechapishwa:
Maandamano makubwa yamezuka jijini Khartoum nchini Sudan baada ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta na kusababisha kupanda kwa bidhaa hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa hilo.
Maandamano hayo yamesabisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa huku waandamanaji wakiharibu na kuchoma magari jijini Khartoum.
Kutokana na maandamano hayo, wizara ya elimu imetangaza kuwa shule zote jijini Khartoum zimefungwa hadi mwisho wa mwezi huu.
Watumiaji wa mitandao ya Internet wanasema kuwa mitandao hiyo imefungwa pia.
Polisi wanasema kuwa wanashikilia waandamanaji zaidi ya ishirini waliokamatwa baada ya kukamatwa wakichoma kituo cha kuuza petroli.
Wananchi wa Sudan wanasema kuwa wataendelea kuandamana hadi pale serikali itakapopunguza bei ya mafuta ambayo imepanda kutoka Pauni 12 nukta 50 za Sudan hadi 20 nukta 80 kwa lita moja.