AFRIKA KUSINI

Afya ya Mandela yaendelea kuimarika akiwa nyumbani

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ameendelea kupata nafuu akiwa nyumbani kwake baada ya kukaa hospitalini kwa karibu miezi mitatu. 

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mjukuu wake Mbuso Mandela amesema kuwa kwa sasa Mandela anaweza kukaa mwenyewe kwenye kitanda chake.

Mandela anaendelea kupatiwa uangalizi wa karibu wa afya yake akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg ambako alirejea baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini mnamo Septemba Mosi.

Mandela alikaa hospitalini mjini Pretoria kwa siku 86 huku afya yake ikitajwa kuwa mbaya lakini imara katika kipindi hicho chote.