Waasi wa M23 watishia kujiondoa kwenye mazungumzo ya amani huko Kampala Uganda
Kundi la Waasi la M23 linalopambana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR limetishia kujiondoa kwenye mazungumzo yanayoendelea nchini Uganda yakiwa na lengo la kutamatisha machafuko yanayoendelea Mashariki mwa taifa hilo.
Imechapishwa:
Kiongozi wa kisiasa wa kundi la waasi la M23 Bertrand Bisimwa ndiye ametangaza kitisho hiyo huku sababu kubwa ambayo ameianinisha ni kwamba jeshi la serikali FARDC limeazisha tena mashambulizi na kushindwa kuheshimu mazungumzo.
Katika hatua nyingine Serikali ya Kinshasa imetangaza kuwaondoa askari wake waliokuwa wamezingira nyumba ya kiongozi wa upinzani Ettien Tchisekedi wa Mulumba tangu mwezi Januari.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC inaendelea kufanya kila linalowezekana katika kuhakikisha eneo la Mashariki mwa Taifa hilo linapata utulivu baada ya kushuhudia machafuko kwa muda mrefu.