RWANDA-Tuhuma

Wafuasi wa chama cha upinzani nchini Rwanda waishio uhamishoni waituhumu Rwanda kusika na kifo cha Patrick Karegeya

Raia wa Rwanda na wanachama wa chama cha upinzani cha RNC (Rwanda National Congress) walikusanyika jana Jumapili kumkumbuka aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Inteljensia nchini Rwanda katika miaka ya 1994 hadi 2004, Patrick Karageya aliyepatika amenyongwa wiki iliyopita jijii Johhanersburg.  

Matangazo ya kibiashara

Raia hao wa Rwanda wamevalia mavazi ya rangi ya zambarau, na kubeba mauwa ya rangi nyeupe mikononi, na kukusanyika katika Ukumbi wa hoteli mjini Johannesburg, ambapo Karegeya alikutwa amenyongwa na watu wasiojulikana Jumatano tarehe mosi Januari mwaka 2014.

Wenye huzuni na hasira dhidi ya serikali ya Kigali ambayo wameamini imehusika katika mauaji ya mpinzani huyo, Familia ya Patrick Karegeya imetangaza atazikwa nchini Afrika Kusini, na si nchini Uganda ambako baadhi ya familia yake wanaishi.

Patrick Karegeya alikuwa anaishi uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2007, baada ya kupoteza imani kwa rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye alikuwa mshirika wake wa karibu.

Upinzani unaituhumu serikali ya Kigali kuhusika na mauwaji hayo, lakini Ubalozi wa Rwanda nchini Afrika Kusini umesema tuhuma hizo ni za kisiasa na hazina ukweli wowote.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Clayson Monyela , amesema kuwa ingekuwa vema kusubiri matokeo ya uchunguzi wa mauaji ya Karegeya badala ya kuanza kutolewa kwa shutuma kama hizo.

Awali, mpinzani mkuu wa utawala wa Rwanda, Kayumba Nyamwasa aliekua mkuu wa majeshi ya Rwanda, ambae kwa sasa anaishi ukimbizini Afrika Kusini, aliituhumu serikali ya Rwanda kuhusika na kifo ya Patrick Karegeya, akibaini kwamba ni mbinu za utawala wa Kigali za kutaka kuwaangamiza wapinzani wake.

Patrick Karegeya na Kayumba Nyamwasa ni miongoni mwa vigogo wa chama tawala cha RPF, ambao wengi ni kutoka kabila la Watutsi waliyowachache nchini Rwanda, waliyoendesha vita vya maguguni hadi kuipindua serikali ya Juvenal Habyarimana, ambayo ilikua ikiundwa na idadi kubwa ya watu kutoka kabila la Wahutu.