ISRAEL-Maandamano

Serikali ya Israel yatoa onyo kali kwa wahamiaji kutoka barani Afrika ambao wanaendelea kuandamana mjini Tel Aviv

Maelfu ya wahamiaji kutoka barani Afrika waliokimbilia Isreal kwa siku ya pili jana Jumatatau waliandamana katika mji wa Tel Aviv kupinga mateso wanayosema wanapata kutoka kwa uongozi wa taifa hilo. Waafrika hao wengi kutoka Sudan, Ethiopia na Eritrea wanalalamikia kuzuiliwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ya kufikishwa mahakamani kufunguliwa mahstaka kwa mujibu wa sera ya uhamiaji nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalianza juzi jumapili.

Waandamanaji hao wengi wao, wanataka kupewa haki ya kufanya kazi huku wakishinikiza serikali kuharakisha maombi yao ya kupewa uraia.

Msemaji mmoja wa serikali alisema kuwa maandamano yao yalifanywa kwa njia ya amani.

"sote ni wakimbizi na ndio tunataka uhuru wala hatutaki kufungwa, '' walisema wahamiaji hao.

Baadhi ya wadadisi wanasema, maandamano yalichochewa na sheria ya kuwazuilia wahamiaji haramu ambayo iliwaondolea matumaini wengi waliotarajia kuwa serikali ingesitisha kabisa msako dhidi ya wahamiaji haramu.

Wahamiaji hao ambao wengi wamekuwa wakiishi Israel kwa miaka mingi na wanaofanya kazi za kipato cha chini, wanasema wote ni wakimbizi ambao wametoroka nchi zao kutokana na mateso.

Wanasema kuwa hali yao sasa kutokana na sheria hiyo watalazimika kuishi jela au kurejea nyumbani.

Kutokana na hatari wanazokabiliwa nazo nyumbani kwao, ina maana kuwa hawawezi kurejeshwa makwao kwa nguvu.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amekemea maandamano hayo na kusisitiza kuwa wahamiaji hao ni haramu, waliingia nchini humo bila ya kufuata sheria na

watarudishwa katika nchi zao.