Afrika Kusini-Rwanda-Uchunguzi

Serikali ya Afrika Kusini yaendelea na uchuguza kuhusiana na kifo cha Patrick Karegeya

France24

Serikali ya Afrika Kusini imeamuru kuharakisha kwa uchunguzi kuhusiana na mauaji ya aliyekuwa mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini Rwanda Patrick KaregeyaMshirika huyo wa zamani wa karibu wa rais Paul Kagame, alikutwa amenyongwa katika hoteli moja mjini Johannesburg tarehe mosi Januari mwaka huu. Polisi nchini Afrika kusini bado haijafanikiwa Kumkamata mtu yoyote, ikiwa ni siku kumi tangu mauaji hayo yatokee na uchunguzi huo kuendelea.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa sheria na wa Ulinzi nchini humo wameitaka tume ya uchunguzi kuwasilisha haraka iwezekanavyo matokeo ya uchunguzi wao,ili watu wafahamu hasa ni nani aliyemuua Karegeya akiwa hoteli jijini Johannerburg.

Aidha, Mawaziri hao wamekariri kuwa Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa pamekuwepo na dalili za mkanganyiko, kauli ambayo imetolewa kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa kifo cha Karegeya.

Serikali ya Kigali tayari imekanusha kuhusika na mauji hayo baada ya kushutumiwa na upinzani kupanga mauji hayo.

Awali Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Rwanda, Kayumba Nyamwasa, ambae iko ukimbizini Afrika Kusini aliinyooshea kidole serikali ya Rwanda kwamba ilihusika kwa kifo cha Patrick Karegeya.

Patrick Karegeya alihudumu kama kuu wa idara ya Ujasusi tangu mwaka 1994 hadi mwaka wa 2005. Hata hivo mkuu huyo wa zamani wa Intelijensia alikua mshirika wa karibu wa rais wa Rwanda Paul Kagame.

Karegeya anatarajiwa kuzikwa baadaye mwezi huu nchini Afrika Kusini.