RWANDA-Siasa

Rais wa Rwanda awatahadharisha wapinzani wake baada ya kifo cha aliekua mshirika wake wa karibu Patrick Karegeya

RFI

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema jana kwamba uhaini una madhara yake, huku akimlenga Patrick Karegeya aliyekuwa afisaa wa idara ya Upelelezi na mtu wa karibu yake, ambaye alikutwa amekufa Januari Mosi katika Hoteli moja huko nchini Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mjini Kigali wakati wa Maombi ya Kitaifa, Rais Kagame alisisistiza kuwa watu walio na tabia ya kuisaliti nchi yake watakiona cha mtima kuni na hawatavumilika, na kuongeza kuwa haiwezekani mtu kubomoa kile wananchi wa Rwanda walichokijenga.

Akizungumzia kifo cha aliyekuwa Kiongozi wa Injteljesnia Patrick Karegeya aliyeuliwa mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini, kiongozi huyo wa Rwanda ameonya kuwa yeyote atakayeendelea kulisaliti taifa hilo atakumbana na mkono wa sheria.

Kauli hiyo ya rais Kagame haikutofautiana na matamshi ya Waziri wake wa Ulinzi James Kabarebe aliyesema kuwa ikiwa mtu anachagua kuwa mbwa, basi atakufa kama mbwa na kuokotwa na kutupwa kama takataka .

Rais Kagame na waziri wake wa ulinzi Kabarebe walikuwa wakimtuhumu Karegeya na wafuasi wake kuanda mfululizo wa mashambulizi ya umwagaji damu kwa kutumia gruneti nchini Rwanda katika miaka ya hivi karibuni.

Rais Kagame amewatahadharisha wafuasi wa Karegeya na wapinzani wake wanaoeshi ugenini kwamba uhaini una madhara yake.

Mwili wa Patrick Karegeya, ambaye alitokea kuwa mpinzani mkubwa wa rais Kagame baada ya kutofautiana, ulikutwa katika chumba kimoja cha Hoteli huku ukionekana aliauawa kwa kunyongwa, ambapo Polisi nchini Afrika Kusini inaendesha uchunguzi, huku upinzani ulio nje ya Rwanda ukiinyooshea kidole serikali ya rais Paul Kagame kuhusika na mauaji hayo.