ZANZIBAR

Zanzibar yaadhimisha miaka hamsini ya mapinduzi

Maadhimisho ya kilele cha sherehe za miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliomaliza utawala wa Kisultani yamefanyika jana katika uwanja wa Amani mjini Unguja ambapo wananchi wengi wamehudhuria kwa wingi sherehe hizo zilizo fana na kupendeza

Matangazo ya kibiashara

Sherehe ambazo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania bara akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wake Dk Mohamed Gharib Bilal, pamoja na ma raisi wa Comoro, Dk Ikililou Dhoinine, muwakilishi wa rais wa china pamoja na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Akiwatolea salaamu na kuwatakia kheri wananchi wa Zanzibar rais wa Comoro Ikililou Dhoinine, amesema Comoro na Tanzania, zina uhusiano mzuri wa karibu na kirafiki tangu kipindi Kirefu.

Upande wake rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema uhusiano wa mataifa hayo haukuanza jana, bali ni wa muda mrefu.

Akiwahutubia wananchi waliofurika kwa wingi Uwanjani hapo rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amesema, wanasherehekea nusu karne ya mapinduzi katika hali ya amani na utulivu. Rais wa Jamuhuri Jakaya Mrisho Kikwete na rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wametangaza tarehe 13 januari kua siku ya mapumziko.