NIGERIA-Diplomasia

Nigeria yaonyooshewa kidole cha lawama kwa kupiga marufuku ndoa za jinsi moja

Mataifa ya Magharibi yanaishtumu Nigeria kwa kupitisha sheria zinazopiga marufuku ndoa za jinsia moja nchini humo. Mataifa hayo yakiongozwa na Marekani yanasema hatua hiyo ya rais Goodluck Jonathan kutia saini sheria hiyo ni kinyume cha haki za binadamu, na ni ya Kibaguzi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesisistiza kuwa Nigeria imeonesha wazi kuwa imekeuka haki za Kimataifa na ahadi iliyotoa kwa ulimwengu mwaka wa 1999 katika Katiba yake kuwa italinda haki ya wanaingeria wote.

Msemaji wa rais Jonathan, Reuben Abatim amesema kuwa kiongozi wa taifa hilo hakuwa na lingine bali kutia saini mswada huo kuwa sheria kutokana na dhana ya wananchi wa taifa lake na watu wa Afrika Magharibi kuwa ndoa za jinsia moja hazifai kwa mujibu wa imani za kidini na tamaduni za waafrika.

Kwa mujibu wa sheria hii mpaya yeyote atakayepatikana akijihusisha na maswala ya ndoa ya jinsia moja atafungwa jela miaka 14.

Sheria hiyo inaweka wazi kuwa ndoa ya mwanamme na mwanamke ndio inayokubakliwa nchini Nigeria.