RWANDA-Siasa

Rwanda yalani muungano kati ya chama cha waziri mkuu wa zamani wa Rwanda na kundi la wanamgambo wa kihutu la FDLR.

Serikali ya Rwanda imelaani vikali muungano wa kisiasa uliofanyika baina ya Chama cha Faustin Twagiranmungu waziri mkuu wa zamani wa Rwanda aliyekimbilia uhamishoni nchini Ubelgiji na makundi ya FDLR na chama cha upinzani cha PS-Imberakuri.Muungano huo unalenga hasa kuiomba Jumuiya ya Kimataifa kushinikiza serikali ya Kigali kuandaa mazungumzo ya kitaifa pamoja na maelfu ya wakimbizi kurejea nchini rwanda. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rwanda imetupilia mbali mapendekezo hayo na kusema kuwa kufanya mazungumzo na watu waliofanya mauwaji ya kimbari ni kuzungumza na shetani.

Olivier Nduhungirehe naibu muakilishi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa, amesema Jumuiya ya Kimataifa imewekea vikwazo waasi wa FDLR ambao wamefanya muungano na Faustin Twagiramungu.

“Faustin Twagiramungu hawezi kuomba Jumuiya ya Kimataifa imsaidie kupata mazungumzo na serikali ya Rwanda wakati ni kundi la wauwaji wa kimbari waliowekewa vikwazo na Jumuiya hiyo kwa njia ya Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo hakutokuwepo na mazungumzo kamwe na FDLR pamoja na wote wanaoafikiana na sera ya mauwaji ya kimbari. Hili ni kosa la kimkakati kwa sababu huwezi kuungana na shetani” amesema Nduhungirehe.

Wakati huohuo, familia ya aliekuwa mkuu wa idara ya ujasusi ambae aliuawa Januari mosi mwaka huu nchini Afrika Kusini Patrick karegeya imeanza kuwasili mjini Johannesburg kwa ajili ya mazishi.

Hata hivyo familia ya Karegeya inaelezea tishio la serikali ya Rwanda kwa wapinzani, kutoridhishwa kwake na uchunguzi unavyoendelea pamoja na mapungufu yanayobainishwa na mmoja wa wanafamilia hao.

David Batenga ambae ni binamu wa Patrick Karegeya, amebaini kwamba ndugu yao akizikwa, baada ya kupata matokeo ya uchunguzi, lakini sivyo ilivyo kutokana na kucheleweshwa kwa uchunguzi huo.

“Tunatishika sana kwa sababu sio ajali ya barabarani ni kitu ambacho kimepangwa kumuuwa mtu na hakihusiani na nchi ya Afrika kusini. Serikali ikikutafuta kwa jambo lolote libaya litakupa tu. Hadi sasa hatujapewa ripoti ya hospitali, na picha za darubini ya hoteli tuone kama kulikuwepo na watu waliofika hapo siku hiyo. Waliokuwepo nchini humu je, wameondoka au? Hayo yote tungetamani kujuwa kabla ya kuzika” amesema Batenga.

Wakati huohuo Marekani imelani mauaji ya Patrick Karegeya, na kauli aliyoatoa hivi karibuni rais wa Rwanda Paul Kagame dhidi ya wapinzani wake, akibaini kwamba yaule atakae jihusisha na uhaini wa taifa la Rwanda atakiona cha mtima kuni.

Awali mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, Kayumba Nyamwasa, ambae yuko ukimbizini Afrika kusini aliinyoshea kidole Serikali ya Rwanda kuhusika na kifo cha Patrick Karegeya, ambae alikua mkuu wa idara ya ujasusi ya Rwanda katika miaka ya 1994 hadi 2005, nabaadae alikimbila ukimbizini afrika Kusini baada ya kupoteza imani kwa rais Paul Kagame.