TANZANIA-Serikali

Baraza jipya la mawaziri nchini Tanzania

Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete RFI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza baraza lake la mawaziri huku akiwahamisha na kuwateua mawaziri na Naibu Mawziri kuziba nafasi zilzioachwa wazi na wale waliojiuzulu. Baraza hilo limekua likisubiriwa na idadi kubwa ya watanzania, lakini baahi ya watanzania wamebaini kwamba uteuzi wa baadhi ya mawiziri haukuwashangaza.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye uteuzi huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na gamu na wananchi wa Tanzania, umeshuhudia mabadiliko machache kwenye baadhi ya wizara huku wale waliolalamikiwa na wabunge wakiendelea kubakia kwenye wizara zao.

Kwenye uteuzi wake rais Kikwete amemteua aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Dr Asha Rose Migiro kuwa waziri wa katiba na sheria, huku wizara ya ulinzi ambaye waziri wake alijiuzulu, ikichukuliwa na Dkt Hussein Mwinyi aliyekuwa wizara ya afya, wakati wizara ya Mambo ya ndani ikichukuliwa na Mathias Chikawe ambapo wizara ya maliasili na utalii ameteuliwa Lazaro Nyalandu aliyekuwa naibu waziri.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanamtazamo chanya kuhusu bararaza hli jipya, wengine wakiwa hawana imani na baraza lenyewe.