Sudani - Mapigano

Jeshi la serikali ya Juba ladai kuurejesha kwenye himaya yake mji wa Malakal kutoka mikononi mwa waasi

vikosi vya serikali ya rais salva Kiir
vikosi vya serikali ya rais salva Kiir REUTERS/James Akena

Jeshi nchini Sudani Kusini limetangaza kurejesha kwenye himaya yake mji wenye utajiri wa mafuta wa Malakal, mji mkuu wa Jimbo la Nil ya Juu baada ya mapigano makali baina yake na waasi tangu mwezi Desemba mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya serikali ya rais Salva Kiir na vile tiifu kwa aliyekuwa makam wa rais wa nchi hiyo Riek Mashar alietumiliwa madarakani mwezi Julai, vimeendelea na mapambano kuwania udhibiti wa mji huo ambao mara kadhaa ulianguka mikononi mwa waasi na kurejea tena mikononi mwa serikali.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameghadhabishwa na hautwa na wanajeshi wa serikali ya Sudani Kusini waliojaribu kumghasi askari wa kulinda amani baada ya kuwakatalia kuingia katika kituo kimoja cha Umoja wa Mataifa ambako wamekimbilia watu zaidi ya elfu kumi.

Hayo yanajiri wakati hatma ya mazungumzo ya mjini Addis Ababa juu ya kutafutwa suluhu ya mzozo huo ikiendelea kufifia huku kila upande ukiendelea kukkota kamba.

Waasi wanaongozwa na Riek Mashar wamendelea kusisitiza kwa serikali ya rais Salva Kiir kuwaacha huru washirika wao wanaozuiliwa katika jela mjini Juba kabla ya kusitisha mapigano, masharti ambayo serikali imeyatupilia mbali.

Juhidi za kuzipatanisha pande mbili zinaendelea kusuasua wakati huu mapingano yakiendelea kuchacha, huku serikali za Kenya na Uganda zikituhumiwa na waasi kuyatuma majeshi yake kuisaidia serikali.