RWANDA-AFRIKA KUSINI-Siasa

Mazishi ya Mkuu wa zamani wa Idara ya Upelelezi wa Rwanda yafanyika nchini Afrika Kusini

Kanali Patrick Karegeya, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi katika miaka ya 1994 hadi 2004
Kanali Patrick Karegeya, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi katika miaka ya 1994 hadi 2004 RFI

Mazishi ya aliyewahi kuwa mkuu wa usalama wa taifa nchini Rwanda Patrick Karegeya na baadae kukimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini kabla ya kuuawa wiki mbili zilizolopita yamefanyika hapo jana jijini Johannesburg. Mkuu huyo wa zamani wa Idara ya Ujasusi katika miaka ya 1994 hadi 2005, alikutwa alifariki katika chumba alichokua alikodi kwenye hoteli moja nchini Afrika Kusini, baada ya upinzani wa utawala ya Paul Kagame kudai kwamba alnyongwa, ukibaini kwa serikali ya Kigali inahusika na kifo hicho.

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 150 walihudhuria mazishi yake huku mjane wa Karegeya, Leah Karegeya akiendelea kusisitiza kuwa anaamini serikali ya Rwanda imehusika kwenye mauaji ya mme wake kutokana na kukosoa sera za utawala wa rais Paul Kagame.

Kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wa rfi aliyeko nchini Afrika Kusini, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Karegeya na wakati fulani alikuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda, Jenerali Kayumba Nyamwasa anasema kuwa haoni kama lengo la Serikali ya Rwanda limefikiwa licha ya mauaji ya rafiki yake.

Kiongozi huyo pia amesisitiza kuwa maadui wa rais Kagame sio maadui wa nchi ya Rwanda kama ambavyo rais Kagame amenukuliwa hivi karibuni akiwatuhumu kuwa wahaini watu wote wanaoipinga Serikali yake.

Jenerali Kayumba Nyamwasa na patrick Karegeya walikua washirika wa karibu wa rais wa Rwanda Paul Kagame.