RWANDA-Sheria

Kesi ya watuhumiwa 16 wa milipuko mjini Kigali yasikilizwa

Kesi ambayo wizara ya ulinzi ya Rwanda imeita “kesi ya ugaidi” , itaanza kusikilizwa hii leo nchini Rwanda ambapo watuhumiwa kumi na sita wakiwemo wanajeshi wazamani wa Rwanda Joel Mutabazi na Innocent Kalisa wanatuhumiwa kujiunga na chama cha RNC cha Patrick Karegeya aliyekuwa mkuu wa intelijensia wa Rwanda katika miaka ya 1994 na 2005 ambae aliyeuawa mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa kundi la wanamgambo wa kihutu wanaopiga kambi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wanafunzi kadhaa wa chuo kikuu cha Rwanda ni miongoni mwa watuhumiwa. Wote hao wanatuhumiwa kushiriki katika mashambulizi tofauti kwa kutumia gruneti nchini Rwanda mwaka 2010.

Innocent Kalisa, aliekutekwa nyara mwezi wa ogasti mwaka jana mjini Kampala, kwa mujibu wa taarifa ziliyotolewa na familia yake, na baadae akakosekana kabisa tangu wakati huo pamoja na Joël Mutabazi , ambae kwa mujibu wa taarifa ziliyotoilewa na shirika la kimataifa linalohudumia wakimbizi HCR, alirejeshwa kutoka Uganda kwenda Rwanda kinyume cha sheria. Msemaji wa jeshi la Rwanda jenerali Joseph Nzambamwita, amesema watu hao ni muhimu sana katika kesi hio.

Innocent Kalisa na Joël Mutabazi ni wanajeshi wa zamani wa kikosi kinachotoa ulinzi wa rais

Wachambuzi wa masuala ya Usalama na Sheria wanazungumzia kesi hiyo kuwa ya kisiasa.

Akiwa ziarani nchini Rwanda, Maïna Kiai mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kufanya mikutano na kuunda mashirika amebaini katika mkutano na waandishi wa habari kwamba viongozi serikalini nchini Rwanda wamekua hawataki raia na vyama vingine vya siasa wasitowe maoni yao kwa kuukosoa utawala.

Utawala wa Paul Kagame umekua ukikosolewa na wapinzani wake ambao waliwahi kushirikiana nae kwa kuuangusha utawala wa Juvenal Habyarimana mwaka 1994, ambao kwa sasa wako ukimbizini katika mataifa ya nje.