BURUNDI-Sheria

Burundi : Mkuu wa chama cha majaji nchini Burundi avuliwa joho lake la kazi

RFI

Mkuu wa chama cha mawakili katika manispaa ya jiji la Bujumbura nchini Burundi, wakili Isidore Rufyikiri, ambae amekua akiukosoa utawala wa Perre Nkurunziza, amefutwa kwenye wadhifa wake akituhumiwa kukiuka maadili ya kazi yake kulingana na kiapo alichoopa wakati alipokabidhiwa uongozi wa chama hicho.

Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo umechukuliwa na korti kuu ya Bujumbura, baada ya mkuu huyo wa chama cha mawakili kutolea wito raia kuandamana kutokana na namna serikali ya Bujumbura haijali raia wake, ameielezea AFP msemaji wa ofisi ya mashtaka, Alice Bangiricenge.

“ Kabla ya kua wakili alikula kiapo, akisema kwamba atajilinda kusema au kuarifu chochote kile ambacho kitakua kinyume na maadili, mambo ambayo yatahusiana na usalama wa taifa, ameedelea kusema bi Alice Bangiricenge, akibaini kwamba almekwenda kinyumee na kiapo hicho.

Isidore Rufyikiri amelani “uamzi huo uliyochukuliwa na majaji kwa manufaa ya serikali ili asaliye kimya, asiendelei kuikemea kwa kutotendea haki raia wake”.

“Niliweka wazi yale ambayo wengine wamekua wakiogopa kutaja, kama vile kuingia katika utawala wa kiimla na kuandwa kwa kundi la wanamgambo ambao wamekua wakiwatishia usalama raia, mfano wa wanamgambo wa kihutu (Interahamwe) kutoka chama kilichotawala nchini Rwanda katika utawala wa Juvenal Habyarimana cha MRND, kabla ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994”, amesema Isidore Rufyikiri.

Alice Bangiricenge, amesema kwamba, ofisi ya mashtaka imemtuhumu wakili Rufyikiri ikiwa na vithibitisho, akikanusha habari zinazosema kwamba majaji wamechukua uamzi huo kwa kuhofiwa kufutwa kazi.

Kesi ya kumfuta kwenye kazi yake ya uakili ilisikilizwa januari 20. Mabalozi wa nchi za magharibi nchini Burundi na zaidi ya mawakili 100 ambao walikua walivalia joho nyeusi kama ishara ya kumuunga mkono, walihudhuria kesi hio.

Lakini Wakili Rufyikiri na mawakili wake walijiondoa katika kesi hio wakipinga dhidi ya namna ya kesi ilivyokua ikiendeshwa, wakisema kwamba ni kinyume na sheria.

Ofisi ya mashtaka ilikua inamtuhumu Isidore Rufyikiri kwamba alitoa maneno ya matusi dhidi ya serikali na viongozi wa ngazi za chini serikalini, baada ya kumuandikia mkuu wa mkoa wa Bubanza (kaskazini-magharibi) jalai 24 mwaka 2013, ambapo ofisi hio ilisema kua barua hio ilikua imejaa maneno ya kuchochea chuki na vurugu.

Isidore Rufyikiri alikua anashtumiwa pia kwamaba katika mkutano na waandishi habari alitolea mwito jeshi, wafanyakazi wa serikali na raia kuandamana hadi kuupindua utawal.

Katika barua yake, wakili Rufyikiri alituhumu utawala kwamba “unataka kumpokonya aridhi m'moja kati ya wateja wake, na kutaka kutumia ubabe kwa kuchukua uamzi”. Katika mkutano na waandishi wa habari,aliwatolea wito raia “kutokubali nchi ya Burundi iwe mikononi mwa vijana wakereketwa kutoka chama madarakani, ambao wamekua wakihusika katika visa vingi vya mauaji”.

Rufyikiri amekua akiungwa mkono na vyama vingi vya kimataifa vya mawakili, mkiwemo shirikisho la vyama vya mawakili nchini Ufaransa na Ubelgiji.