AFRIKA KUSINI

Wafanyakazi wa migodi nchini Afrika Kusini wagoma kurejea kazini

REUTERS/Mike Hutchings

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa mgodini nchini Afrika Kusini wameendelea kusisitiza kubaki kwenye mgomo wao hata kwa zaidi ya mwezi mmoja ikibidi mpaka pale watakapopata suluhu na waajiri wao.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo baina ya viongozi wa wafanyakazi na waajiri hayajaonekana kufua dafu baada ya kukataa mapendekezo mapya ya nyongeza ya mishahara yaliyotolewa.

Kiongozi wa wafanyakazi hao Jimmy Gama amesema majadiliano zaidi yanatarajiwa kuendelea leo jumamosi katika jitihada za kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Vyama vya wafanyakazi wa migodi vinataka mshahara wa kima cha chini iwe randi 12,500 sawa na Dola 1,150, kiasi ambacho ni mara mbili ya mishahara ya sasa.

Madai kama hayo ndiyo yaliyochochea migomo katika sekta ya madini mwaka 2012 ambapo polisi waliwapiga risasi na kuwaua wachimba migodi 34 katika mgodi wa Marikana.