AFRIKA-Soka

Michuano ya soka ya klabu bingwa barani Afrika yarindima kwenye viwanja vya baadhi ya mataifa ya Afrika

Wachezaji wa club AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Wachezaji wa club AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo RFI

Michuano ya soka ya klabu bingwa barani Afrika inaanza mwishoni mwa juma hili katika mataifa mbalimbali barani Afrika. Hii ni michuano ya awali, jijini Dar es salaam nchini Tanzania, Yanga watakuwa katika uwanja wa taifa wa Dar es salaam kumenyana na Komorozine Sports kutoka Comoros.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Kenya, mabingwa wa ligi msimu uliopita Gor Mahia watamenyana na US Bitam ya Gabon mechi itakayochezwa jijini Nairobi.

Klabu ya Baraza la jiji la Kampala, KCC watakuwa jijini Khartoum nchini sudan kumenyana na wenyeji wao Al Merreikh.

Siku ya Jumapili, AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa nyumbani kumaliza kazi na Kano Pillars ya Nigeria huku AC Leopards ya Congo Brazivile ikiwa karibisha Rayon Sport ya Rwanda.

Mashabiki wa soka Afrika Mashariki na Kati watakuwa wanafuatailia michuano hii kwa karibu sana hasa baada ya vilabu vingi katika siku za hivi karinbuni kuondolewa mapema katika kinyanganyiro hiki.