Misri

Morsi awataka wafuasi wake kuendeleza harakati za mapinduzi nchini Misri

Rais wa Misri Mohamed Morsi
Rais wa Misri Mohamed Morsi rfikiswahili

Rais aliyeondolewa madarakani na jeshi nchini Misri Mohamed Morsi, ametoa wito kwa wafuasi wake kuendeleza harakati zao za mapinduzi, wakati huu harakati za kudai kurejeshwa kwake madarakani zikipotelea katika sura ya ukandamizwaji mkubwa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Morsi ametoa wito huo wakati wa kesi yake kuhusu madai ya kuvunjwa kwa gereza na mashambulizi dhidi ya polisi, huku mahakama nyingine ikiwaachia huru maafisa sita wa polisi waliokuwa wakishutumiwa kwa kuwaua waandamanaji wakati wa mapinduzi uasi ya mwaka 2011 dhidi ya mtangulizi wake Hosni Mubarak.

Wakati huo huo, watu wenye silaha wameripotiwa kumwua afisa mwandamizi wa usalama ambaye alishiriki katika kuandaa ripoti dhidi ya viongozi wachama cha Muslim Brotherhood.

Kundi la Brotherhood bado linafanya maandamano ya kila wiki dhidi ya serikali licha ya ukandamizaji mkubwa ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,400 tangu jeshi lilipompindua rais Morsi mwezi Julai, baada ya mwaka mmoja tu kukaa madarakani .