SOMALIA-AL SHABAAB

Al Shabab yakiri kuhusika na shambulizi la bomu nchini Somalia jana Alhamisi

Wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia
Wanamgambo wa Al Shabab nchini Somalia AFP

Kundi la Al Shabab nchini somalia limetangaza kuwa linahusika na bomu la kutegwa kwenye gari lililolipuka jana na kusababisha vifo vya watu saba mjini Mogadishu likiwa limelenga askari wa jeshi la ulinzi karibu na mgawaha ulio karibu na makao makuu ya usalama wa taifa.

Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini Somalia wamesema kuwa watu saba wameuawa wakati watu walioshuhudia tukio hilo la mlipuko wa bomu wamesema kuwa idadi ya watu waliokufa ni watu nane.

Shambulio hilo la bomu ni mwendelezo wa matukio kama hayo ambayo kundi la AL shabab limekuwa likiyafanya katika majengo ya serikali mjini Mogadishu nchini Somalia.

Shambulio hilo la bomu ni la karibuni katika mashambulizi mengi katika mji huo hatari, ambako kundi la Al Shabab lenye uhusiano na kundi laAl Qaeda linapigana kuiangusha serikali inayoungwa mkono kimataifa.

Mashambulizi ya karibuni ya Al Shabab yamelenga maeneo muhimu ya serikali na vikosi vya usalama, katika jitihada za wazi za kuharibu sifa za madai ya serikali kwamba imeshinda vita dhidi ya wapiganaji wa kiislam.