RWANDA

Rwanda yalaani mahakama nchini Ufaransa kukataa kuwarejesha nchini mwao watuhumiwa wa mauaji ya kimbari

Watuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Claude Muhayimana na Innocent Musabyimana
Watuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Claude Muhayimana na Innocent Musabyimana fr.igihe.com

Serikali ya Rwanda imelaani vikali hatua ya mahakama moja nchini Ufaransa, kukataa kuwarejesha nchini humo raia wake watatu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda. 

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa mahakama hiyo unabatilisha hukumu ya awali ambayo ilitolewa na mahakama ya rufaa mwezi November mwaka jana kuruhusu kurejeshwa nyumbani kwa watuhumiwa, Claude Muhayimana na Innocent Musabyimana.

Mahakama hiyo pia imetengua uamuzi wa awali wa kurejeshwa nyumbani kwa kanali wa zamani kwenye jeshi la Rwanda, Laurent Serubuga anayetakiwa na Serikali ya kigali alkihusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Balozi wa Rwanda nchini Ufaransa, amekosoa uamuzi huo akidai Ufaransa imeendelea kuwalinda watu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji yao lakini akaonesha imani yake kuwa watashtakiwa kwenye mahakama za Ufaransa.