SOMALIA-SHAMBULIO

Kundi la wanamgabo la Al Shabab lajigamba kutekeleza shambulio liliyogharimu maisha ya watu 11

Mabaki ya gari aliyokuwemo mshambuliaji mbele ya  hotel Jazeera mjini Mogadiscio
Mabaki ya gari aliyokuwemo mshambuliaji mbele ya hotel Jazeera mjini Mogadiscio VOA

Mshambuliaji wa kujitowa muhanga aliyejilipuwa jana jumnne katika mji wa Bula Burde ulionyakuliwa hivi karibuni kuotoka mikononi mwa wanangmabo wa Alshabab alikuwa ni raia wa Norway mwenye asili ya somalia ambaye alikuwa na umri wa miaka 60.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Al Shabab Abdulaziz Abu Musab ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 60 anatambulika kwa jina la Abdullahi Ahmed Abdulle ambaye alijiunga na Al Shabab kutoka Norway kwa ajili ya kupambana na maadui wa Allah.

Msemaji huyo wa Al Shabab amesema mzee huyo amejitolea kwa ajili ya Allah, ikiwa ni ishara kwamba jihad haina umri.

Hapo jana, mshambuliaji wa kujitowa muhanga ambaye alikuwa katika gari, alijilipua kwenye hoteli ambapo askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika Amisom kutoka nchini Djibouti walikuwa wamepiga kambi katika mji wa Buula Burde kwenye umbali wa kilometa 200 na jiji la Mogadishu na kusababisha vifo vya askari kadhaa katika tukio hilo.

Mji wa Buula Burde ulikombolewa kutoka mikononi mwa Al shabab March 13 mwaka huu baada ya majeshi ya Amisom kufanya mashambulizi makubwa na kuwafurusha wanamgambo wa Al Shabab katika mji huo.

Kundi la wanamgambo wa alshabab limekuwa likipata pigo kubwa ya kiupoteza miji muhimu iliokuwa ikikalia tangu mwezi Agosti mwaka 2001 wakati ilipoanzishwa operesheni ya Amisom dhidi ya wanamgambo hao ambapo hatuwa ya kwanza ilikuwa ni kufurushwa katika mji wa Mogadishu.

Licha ya kupoteza miji kadhaa, kundi hilo la Alshabab bado linashikilia maeneo kadhaa ya vijijini na sasa wanapambana kwa kutumia mbinu za kuendesha mashambulizi ya kujitowa muhanga katika jiji la Mogadishu.