Misri-Mauji

Milipuko miwili yatokea nchini Misri na kumuuawa jenerali mmoja wa Polisi jijini Cairo

Jenerali mmoja wa polisi apoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga April 2
Jenerali mmoja wa polisi apoteza maisha katika shambulio la kujitowa muhanga April 2 REUTERS/Al Youm Al Saabi Newspaper

Kumetokea milipuko miwili tofauti jijini Cairo Misri kwenye uwanja wa chuo kikuu cha Cairo na kusababisha kifo ha jenerali mmoja wa polisi na kujeruhi watu kadhaa, kwenye mfulilizo wa matukio yanayolenga vyombo vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Polisi mjini cairo wamethibitisha kutokea kwa milipuko miwili ya bomu kwa nyakati tofauti kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Cairo ambapo watu waliotekeleza shambulio hilo walimlenga naibu waziri wa ulinzi.

Polisi wamesema kuwa kwenye shambulio la kwanza afisa mmoja wa juu wa jeshi la Polisi aliuawa wakati mlipuko wa pili ulilenga msafara wa naibu waziri wa Ulinzi na kumjeruhi, tukio ambalo polisi wanadai limetekelezwa na makundi ya kiislamu yanayomuunga mkono Mohamed Morsi.

Wakati polisi na waandishi wa habari wakikusanyika kwenye eneo la tukio kushuhudia kile kilichotokea kwenye milipuko miwili, kulitokea tena mlipuko wa tatu karibu kabisa na geti kuu la kuingia kwenye chuo kikuu cha Cairo na kujeruhi watu kadhaa.

Toka kuondolewa madarakani kwa Mohamed Morsi na jeshi la nchi hiyo, wanamgambo wa kiislamu wameongeza mashambulizi zaidi dhidi ya vikosi vya usalama, mashambulizi yanayokuja ikiwa imepita wiki moja tu toka Jenerali Abdel Fattah al-Sisi atangaze kuwania kiti cha urais na kujiuzulu nafasi zake.