SUDANI KUSINI-MAREKANI-Vikwazo

Marekani imetoa onyo kwa wanaochochea vita Sudani Kusini

Rais wa Marekani Barack Obama, akitoa onyo kwa wale wanaochochea machafuko nchini Sudani Kusini.
Rais wa Marekani Barack Obama, akitoa onyo kwa wale wanaochochea machafuko nchini Sudani Kusini. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Barrack Obama amesema serikali yake itamwekea vikwazo yeyote atakayebainika, kuchochea machafuko nchini Sudan Kusini, kuvamia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa pamoja na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Obama ameagiza kuwa watu hao kutoka upande wa serikali au waasi kuwekewa vikwazo vya kusafiri na mali zao kuzuiwa, imebaini ikulu ya Marekani.

Hatua hii ya inakuja majuma mawili baada ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuoya serikali ya sudani Kusini na waasi kwamba huenda wakachukuliwa vikwazo iwapo hakuatakua na maandeleo yoyote katika mazungumzo kati yao na kuheshimu makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyoafikiwa mjini Addis Ababa, chini Ethiopia.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Jay Carney, amethibitisha katika tangazo liliyotolewa na ikulu hio kwamba mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi yanaweza kulitumbukiza taifa hilo changa, liliyopata uhuru wake mawaka wa 2011 kwa usaidizi wa Marekani.

“Marekani haitokaa kimya wakati viongozi watarajiwa wa taifa la Sudani Kusini wanaweka mbele maslahi yao binafsi kuliko maslahi ya raia na taifa lao”, amesema Carney.

Jay Carney ameitaka serikali ya Sudani Kusini na waasi wanaoongozwa na aliyekua makamu wa rais Salva Kiir, Riek Machar kuwasiliana haraka iwezekanavyo na kuheshimu mchakato wa amani.

Mazungumzo ya amani yamevunjika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia baada ya serikali ya Juba kukataa kushirkishwa kwa wanasiasa saba wa upinzani katika mauzungumo hayo yanayoongzwa na wasuluhishi wa IGAD.

Machafuko hayo yaliyotokea nchini Sudani Kusini desemba 15 katika mji mkuu wa taifa hilo, Juba, yamesababisha maelfu ya watu kuuawa na wengine wanaokadiriwa kuwa sawa na 900.000 kulazimika kuyahama makaazi yao.