RWANDA-Mauaji ya kimbari

Miaka 20 ya mauaji ya kimbari Rwanda,Mjumbe wa Marekani Samantha Power kuhamasisha umoja Rwanda,Burundi

Maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari Rwanda,Mjumbe wa Marekani Samantha Power kuhamasisha umoja Rwanda,Burundi
Maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari Rwanda,Mjumbe wa Marekani Samantha Power kuhamasisha umoja Rwanda,Burundi REUTERS/Eduardo Munoz

Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power atafanya ziara nchini Rwanda, Burundi, na Jamuhuri ya Afrika ya kati kuanzia kesho April 6 wakati nchi ya Rwanda ikianza maadhimisho ya mika 20 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda yaliyotokea mwaka 1994.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Marekani katika Umoja wa mafaita UN umearifu kuwa akiwa mjini Kigali nchini Rwanda Samantha Power ataongoza ujumbe wa Marekani katika maadhimisho hayo ambayo takribani watu laki nane wengi wao watutsi waliuawa.

Katika hatua nyingine taarifa hiyo imebainisha Samantha Power atazuru nchi jirani ya Burundi ambako kuna hofu ya kuzuka kwa tofauti za kikabila ambapo Samantha atakutana na raisi Nkurunziza na wanafunzi na viongozi wa kiraia kujadili namna ya kuepukana na chuki za kikabila na kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005.

Ziara ya Bi Samantha itatamatika huko Jamuhuri ya Afrika ya kati ambapo atakutana na wanachama wa serikali mpya ya mpito, ikiwa ni pamoja na Rais Catherine Samba-Panza na uongozi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika .