DRC-Volkano

Shughuli nzito huenda zikasababisha mlipuko wa Volkano nchini DRC hivi karibuni

Mlipuko wa volkano mlima Nyamulagira mwaka 2010
Mlipuko wa volkano mlima Nyamulagira mwaka 2010 AFP / GorillaCD

Imeelezwa kuwa mlipuko wa volkano huenda ukatokea katika siku chache zijazo nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kufuatia kushuhudiwa kwa shughuli nzito nchini humo,taasisi ya uangalizi wa Volkano mjini Goma (OVGoma) imearifu.

Matangazo ya kibiashara

Wataalam wanasema shughuli zinazochochea tetemeko la ardhi na mlipuko wa volkano kwenye Mlima Nyamulagira, mashariki mwa nchi hiyo, kwa sasa haziwaweki hatarini wakaazi, ingawa mji wa Goma wenye watu zaidi ya milioni uliathiriwa na mlipuko mwaka 2002, ukiwa umbali kilometa 20 tu.

Wanasayansi wanasema shughuli za kivolkano hazipaswi kuathiri mlima wa volkano wa Nyiragongo, ambao uliripuka miaka 12 iliyopita.

Mji wa Goma ambao upo mpakani mwa DRC na Rwanda, umo hatarini kutokana na kuwa katikati ya milima miwili ya volkano .

Mlipuko wa mwaka 2002 ulisababisha mito na miamba kuyeyuka na kuharibu majengo na kuacha maelfu ya watu bila makazi.