TANZANIA-Mafuriko

Mafuriko yasababisha maafa na hasara kubwa nchini Tanzania

Mji wa Dar es Salaam ukikumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazonyesha, aprili 12 mwaka 2014, picha hii ni baada ya mafuriko.
Mji wa Dar es Salaam ukikumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazonyesha, aprili 12 mwaka 2014, picha hii ni baada ya mafuriko. WISSING Claire/RFI

Mvua ambazo zinaendelea kunyesha nchini Tanzania, hususan katika mikoa ya Morogoro, Lindi na jiji la Dar es Salaam, na kusababisha hasara kubwa mkiwemo vifo uharibifu wa mazingira na baadhi ya madaraja yamevunjwa kutokana na mvua hizo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na RFI Kiswahili, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Mek Sadik amesema kuwa mafuriko hayo pia yameharibu barabara na hivyo kutatiza usafiri wa kuingia na kutoka Dar es salaam baada ya madaraja kadhaa kuvunjika na barabara kujaa maji.

Serikali ya Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikiendelea kutoa wito kwa watu wanaoishi mabondeni kuhama makwao ili kuepuka makaazi yao kusombwa maji bila mafanikio.

Mafuriko haya yameyakumba hata baadhi ya mikoa nchini na kusababisha maafa.
Watoto watano wamekufa maji katika maeneo mbalimbali mkoani Morogoro na mwingine Dar es Salaam jana baada ya kutumbukia kwenye mito na mashimo yaliyofurika maji ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Vifo hivyo vinafanya idadi ya watu walipoteza maisha tangu mvua hizo kubwa zilipoanza Aprili 10, mwaka huu kufikia zaidi ya 10 na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara, makazi ya watu na mazao.