NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

UN imelani mauaji ya watu zaidi ya 70 nchini Nigeria

Shirika la msalaba mwekundu na mashirika mengine ya kihisani yakisafirisha hospiatlini miili ya watu waliyouawa baada ya shambulio liliyotokea jana, aprili 14 mwaka 2014.
Shirika la msalaba mwekundu na mashirika mengine ya kihisani yakisafirisha hospiatlini miili ya watu waliyouawa baada ya shambulio liliyotokea jana, aprili 14 mwaka 2014. REUTERS/Afolabi Sotunde

Siku moja baada ya wanaodaiwa kuwa ni wanamgambo wa kundi la kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria kutekeleza shambulio la bomu kwenye mji mkuu Abuja na kuua watu zaidi ya 70, jumuiya ya kimataifa imelaani shambulio na kutaka hatua kuchukuliwa kuwadhiti wanamgambo hao.  

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa kupitia kwa katibu mkuu wake Ban Ki Moon pamoja na nchi ya Marekani na Uingereza wamelaani shambulio hili ambalo wameliita la kibinafsi na lililokosa utu kwakuwa liliwalenga wananchi wasio na hatia.

Watu 71 waliuawa mapema jana asubuhi na wengine 124 walijeruhiwa katika mashambulizi tofauti ya mabomu yaliyotokea kwenye kituo cha magari, nje kidogo na mji wa Abuja, polisi imethibitisha.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamekua kitisho kwa usalama wa Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamekua kitisho kwa usalama wa Nigeria. Reuters/Tiksa Negeri/Files

Punde baada ya kutembelea eneo la tukio, rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema serikali yake haitakatishwa tamaa dhidi ya vita vya kulitokomeza kundi hili licha ya siku za hivi karibuni kushuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji hawa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa na Usalama wanaona kuwa mashambulizi ya kundi la Boko Haram hayatakoma kwakuwa suluhu dhidi ya kundi hilo haijapatikana mpaka sasa.

Taifa la Nigeria limekua likikumbwa mara kwa mara na na mashambulizi ya mabomu, na kusababish vfo vingi, na watu wengine kujeruhiwa.

Mwaka wa 2010 gari liliyobeba vilipuzi lililipuka na kuua watu 12 na wengine 38 kujeruhiwa karibu na eneo la Eagle Square, ambako zilifanyika sherehe za miaka 50 za uhuru wa Nigeria.

Kundi linalotetea kujitenga kwa jimbo la Niger Delta (mend) lilikiri kuhusika na shambulio hilo la kwanza kutokea katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Tangu wakati huo taifa hilo likabiliwa na mashambulizi ya hapa na pale na kusababisha vifo.

Watu zaidi ya 500 wanaarifiwa kuuawa katika mashambulizi kama hayo tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014.