SOMALIA-Mashambulizi

Somalia: Wabunge walengwa na mashambulizi

Kundi la al Shabab laonya wabunge wa Somalia, baada ya kutekeleza mauaji ya wabunge wawili mjini Mogadiscio.
Kundi la al Shabab laonya wabunge wa Somalia, baada ya kutekeleza mauaji ya wabunge wawili mjini Mogadiscio. AFP / A. Abdulle Abikar

Mbunge wa Somlia ameuawa kwa kupigwa risase mapema leo asubuhi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadiscio, polisi imearifu. Mauaji hayo yananafuatia mauaji ya mbunge mwengine ambae aliuawa jana katika shambulio la bomu liliyokua limetegwa ndani ya gari lake. Wanamgambo wa kislamu wa kundi la al Shabab wamekiri kutekeleza matukio yote mawili ya mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Abdi Aziz Asak Mursal ameuawa karibu na nyumba yake inayopatikana katika mtaa wa Madina, kusini mwa mji wa Mogadiscio, na watu wawili ambao baada ya kitendo hicho walitimka.

“Hatuna taarifa zaidi, lakini kinachofahamika tu ni kwamba mbunge ameuawa”, askari polisi ambaye anajulikana kwa jina la Mohamed Dalane ameielezea AFP, huku akibaini kwamba marehemu alipigwa risase nyingi na kufariki papo hapo.

Wanamgambo wa kislamu wa kundi la al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo, kama walivyokiri kuhusika na mauaji mengine ya mbunge Isak Mohamed Ali, ambae aliuawa jana jumatatu na kumjeruhi rafiki yake Mohamedi Abdi.

“ Tumehusika na mauaji ya mbunge huyo dhalimu ambae anatetea maslahi ya wageni”, amesema Abdul Aziz Abu Musab, msemaji wa kundi la al Shabab akiambia AFP, huku akibaini kwamba huo ni ujumbe ambao unaelekezwa kwa wanasiasa wengine madhalimu ambao wanadai kuwa ni serikali ya Somalia.

Siku moja kabla, msemaji huyo wa kundi la al Shabab, alisema kwenye kituo cha redio inayomilikiwa na al Shebab kwamba wanamgambo wa kundi hilo “walilenga na kumuua mtu anaedai kuwa ni mbunge na kumjeruhi mwengine”.

Madhalimu hao wanasaidia watu wasiyokua ndugu zetu kiimani”, ameendelea kusema Musab, huku akionya kuwa wabunge wote wanalengwa na wanamgambo wa kislamu wa al Shabab, na watauawa mmoja mmoja.

Hali inayojiri chini Somalia
Hali inayojiri chini Somalia © AFP / Ibrahim Elmi

Wanamgambo wa kundi la al Shabab walionya mwishoni mwa mwezi wa septemba mwaka 2012 kwamba watawaua mmoj mmoja wabunge wa bunge jipy la Somalia.

Mbunge mwengine, Feisal Warsame Mohamed aliuawa mwezi wa desemba katika shambulio la bomu liliyotegwa chini ya kiti cha gari. Gari ya ya mbunge mwengine Cheikh Adan Mader ililipuliwa kwa bomu mwezi wa jualai mwaka 2013, lakini mbunge huyo akanusurika.

Kundi hilo la al Shabab lilipoteza maeneo mengi kusini na katikati mwa Somalia, ambayo yalikua chini ya himaya yao tangu wanamgambo wake walipotimuliwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadiscio mwezi wa ogasti mwaka 2011.