Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Usalama

Wafanyakazi 22 wa shirika la MSF wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vifaru vya wanajeshi wa Ufaransa wanaolinda amani katika miji ya  Bouar na Bossembélé (Jamhuri ya Afrika Kati).
Vifaru vya wanajeshi wa Ufaransa wanaolinda amani katika miji ya Bouar na Bossembélé (Jamhuri ya Afrika Kati). Photo : Olivier Fourt / RFI
Ujumbe kutoka: RFI
3 Dakika

Watu wapatao 22 wakiwemo viongozi 15 na wafanyakazi watatu wa shirika la kibinadamu la Médecins Sans Frontières wameuawa katika shambulio liliyoendeshwa na watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa waasi wa zamani wa Seleka, afisa mmoja wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Misca) amethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limeendesha dhidi ya hospitali moja katika kijiji kimoja kwenye umbali wa kilomita 450 kaskazini mwa mji wa Bangui.

“Watu wenye silaha kutoka kundi la waasi wa zamani na wengine kutoka jamii ya Peul walishambulia juzi jioni hospitali moja inayodhaminiwa na shirika la Madaktari wasiyo na Mipaka la MSF katika jimbo la Nanga Boguila, na kuua watu 22, miongoni mwao watu watatu wenye uraia wa jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao walikua waliajiriwa kwenye shirika hilo la MSF”, amesema afisa huyo. Shirika la Madaktari wasio na mipaka MSF nchini Uholanzi limethibitisha kuuliwa kwa viongozi watatu wa shirika hilo.

Hayo yakijiri machafuko kati ya waasi wa zamani wa seleka, ambao wengi wao ni watu kutoka jamii ya waislamu na wanamgambo wa kundi la kikristo la Anti-balaka yanaendelea nchini Jamhuri ya Afrika Kati, na kusababisha waislamu, ambao idadi yao ni ndogo ikilinganishwa na jamii zingine,kuyahama makaazi yao.

Wanajeshi wa Kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) wakiwahamisha watu kutoka jamii ya waislamu kutopka katika mtaa wa PK12, katika wa Bangui, aprili 27 mwaka 2014.
Wanajeshi wa Kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) wakiwahamisha watu kutoka jamii ya waislamu kutopka katika mtaa wa PK12, katika wa Bangui, aprili 27 mwaka 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Watu takriban 1300 kutoka jamii ya waislamu wamelazimika kuondoka jana mji wa Bangui wakisafirishwa na magari ya mashirika ya kihisani yakishindikizwa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca).

Watu hao wamepelekwa kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Watu kutoka jamii ya waislamu mjini Bangui na maeneo mengine ya Afrika ya Kati wamekua wakishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa kundi la kikristo la Anti-balaka, kundi ambalo Kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika kilitangaza hivi karibuni kuendesha vita dhidi yake.

Serikali imeelezea maskitiko yake jana jioni kuhusu zoezi hilo la kuwahamisha raia hao kutoka jamii ya waislamu, ikisema kwamba haikushirikishwa na limeendeshwa bila ridha yake.

Waziri wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwenye dhamana ya maridhiano, Antoinette Montaigne.
Waziri wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwenye dhamana ya maridhiano, Antoinette Montaigne. REUTERS/Siegfried Modola

Wanamgambo wa kundi la kikristo la Anti-balaka wamekua wakidai kwamba wamekua wakijilipiza kisase kwa ndugu zao waliyouawa na waasi wa zamani wa Seleka, ambao wengi wao ni kutoka jamii ya waislamu walipokua madarakani tangu mwezi machi mwaka 2013 hadi januari mwaka 2014.

Katika mtaa wa PK-12, watu 18 waliuawa baadhi kwa risase, gruneti, na wengine kwa mapanga tangu mwezi desemba, huku idadi ya watu waliyojeruhiwa ikiwa kubwa, wamethibitisha watu kutoka jamii ya waislamu, na majirani kutoka makabila mengine wanaoeshi katika mtaa huo wa PK-12.

Machafuko yaliyosababishwa na kundi la Anti-balaka na Seleka yanakuza uhusiano mbaya kati ya jamii ya warito na jamii ya waislamu, ambazo ziliishi vizuri kwa miongo kadhaa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.