UN-Sudani Kusini-Mauaji ya kimbari

UN haitokubali mauaji ya kimbari yatokeye Sudani Kusini

Mkuu wa masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Navy Pillay, akiwa ziarani nchini Sudani Kusini.
Mkuu wa masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Navy Pillay, akiwa ziarani nchini Sudani Kusini. REUTERS/Denis Balibouse

Umoja wa Mataifa Umeonya pande zinazohusika katika mgogoro wa Sudani Kusini kwamba watahusishwa katika machafuko yanayoshuhudiwa nchini humo, na kufahamisha kwamba hautokubali mauwaji ya kimbari yatokeye katika taifa hilo changa.

Matangazo ya kibiashara

“Machafuko yanayoshuhudiwa nchini Sudani Kusini , wito wa kukuza chuki na mauaji ambavyo vinaonekana kuchukua na fasi, huku viongozi wa Sudani Kusini pamoja na jumuiya ya kimataifa wakifumbia macho hali hio, ambayo inaonekana kua tishio kwa usalama wa wataifa na raia wake”, amesema Navi Pillay, mkuu wa masuala ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, ambaye yuko ziarani nchini Sudani Kusini.

Mapigano kati ya jeshi linalomuunga mkono rais Salva Kiir na waasi watiifu kwa aliekua makamu wa rais Riek Machar, ambayo yalianza tangu desemba 15, yamesababisha mzozo wa kijamii kati ya jamii mbili ya Dinkakabila ya Salva Kiir) na Nuer (kabila ya Riek Machar).

Mauaji ya raia ya hivi karibuni yaliyotokea katika miji ya Bentiu (kaskazini mashariki) na Bor (mashariki) ni ishara kwamba taifa la Sudani Kusini liko mbioni kukumbwa na mauaji ya kimbari, amebaini Pillay.

Watoto waliyokimbia mapigano katika mji wa Bor, wakipewa hifadhi katika kambi iliyojengwa kwenye eneo la Umoja wa Mataifa la Mingkaman,
Watoto waliyokimbia mapigano katika mji wa Bor, wakipewa hifadhi katika kambi iliyojengwa kwenye eneo la Umoja wa Mataifa la Mingkaman, REUTERS/Kate Holt/UNICEF

Wito wa kukuza chuki, mauaji yenye misingi ya kikabila vinatia hofu kwamba machafuko haya yanaweza kulitumbukiza taifa la Sudani Kusini katika mauaji ya Kimbari, iwapo jumuiya ya kimataifa hawatowajibika hasa kukomesha machafuko haya yanayoendela, amesema Adama Dieng, mshauri maalumu kwenye Umoja wa Mataifa.

Wanamgambo wa kihutu wakiwa katika mazoezi, julai 27 mwaka 1994 mjini Butare, nchini Rwanda.
Wanamgambo wa kihutu wakiwa katika mazoezi, julai 27 mwaka 1994 mjini Butare, nchini Rwanda. AFP / HOCINE ZAOURAR

Amebaini kwamba Umoja wa Mataifa uko mbioni kuchukua hatua zinazohitajika ili kuwalindia usalama raia wa Sudani Kusini, ambayo inafananishwa na taifa la Rwanda liliwapoteza raia wake takriban 800.000 waliyouawa katika mauaji ya kimbari mwaka 1994, ambao wengi wao walikua ni kutoka jamii ya watutsi, na Umoja wa Mataifa haukuweza kuzuia mauaji hayo yasitokeye.

Machafuko ya Sudani Kusini yamesababisha maefu ya raia kupoteza maisha na maelfu wengine kyahama makaazi yao.