UBELGIJI-BURUNDI-Sheria

Kingozi wa upinzani Burundi Alexis Sinduhije akamatwa Brussels

Alexis Sinduhije wakati wa mkutano wa chama chake cha MSD mjini Bujumbura, aprili 11 mwaka 2010.
Alexis Sinduhije wakati wa mkutano wa chama chake cha MSD mjini Bujumbura, aprili 11 mwaka 2010. AFP PHOTO/Esdras Ndikumana

Kiongozi wa chama cha upinzani cha MSD nchini Burundi Alexis Sinduhije amekamatwa jana asubuhi nchini Ubelgiji. Alexis Sinduhije amekamatwa katika uwanja wa ndege Zaventem mjini Brussels nchini Ubelgiji wakati alikua akitokea katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Burundi walitoa mwishoni mwa mwezi machi hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa upinzani, akituhumiwa kuanzisha vuguvugu dhidi ya utawala wa Pierre Nkurunziza.

Alexis Sinduhije anachukuliwa na serikali ya Bujumbura kwamba alihusika na machafuko yaliyotokea mwezi machi kati ya wafuasi wake na polisi.

Wakili wake Bernard Maingain amelani mazingira ya kukamatwa kwa mteja wake na amri iliyotolewa na serikali ya Ubelgiji ya kumrejesha nchini mwake.

Inasadikiwa kuwa maafisa wa idara ya uhamiaji ya Ubelgiji walitoa taarifa kwa ubalozi wa Burundi nchini humo, ambao papo hapo uliwasilisha kwa maafisa hao hati ya kukamatwa kwa Alexis Sinduhije.

“Hali ya sintofahamu ilishuhudiwa jana alaasiri baada ya kutokea mabishano kati ya viongozi wa Ubelgiji na ubalozi wa Burundi, kwani ubalozi huo wa Burundi ulipewa taarifa, kwa mujibu wa habari ambazo ninazo, viongozi wa Ubelgiji walipewa taarifa kuhusu hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Alexis Sinduhuije”, amesema wakili Bernard Maingain.

Kwa muijbu wa msemaji wa wizara ya maambo ya nje ya Ubelgiji, Alexis Sinduhije atabaki nchini Ubelgiji sehemu anako ziwiliwa kwenye uwanja wa ndege hadi yatakapotolewa maamuzi mapya.

Msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Ubelgiji amebaini kwamba kumekua na mazungumzo kati ya wizara yake na ile ya mambo ya ndani, huku akikiri kwamba suala hili ni lenye utata, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

Burundi inajiandaa kwenye uchaguzi mkuu mwaka ujao katika mazingira ya kutatanisha kisiasa, kwani hivi karibuni, Umoja wa mataifa ulitoa onyo kali kwa serikali ya Burundi na kuitaka ijirekebishe kwa tuhuma zinayoikabili, hususan kugawa silaha kwa vijana wa chama tawala cha Cndd-fdd, kuminya uhuru wa kujieleza, kupiga vita mikutano ya hadhara, kukandamiza wapinzani,...