Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Matukio yaliyojiri Duniani wiki hii yakigubikwa na migogoro ya kisiasa

Sauti 21:34
Raisi wa Sudan kusini Salva Kiir (Kushoto) pamoja na Raisi mwenza wa Kenya Uhuru Kenyatta (Kulia.), wakiwa Juba, tarehe26 desemba 2013.
Raisi wa Sudan kusini Salva Kiir (Kushoto) pamoja na Raisi mwenza wa Kenya Uhuru Kenyatta (Kulia.), wakiwa Juba, tarehe26 desemba 2013. REUTERS/Hakim George

Wajumbe wa Serikali ya Sudan Kusini walikutana na wawakilishi wa kundi la wapiganaji walio tiifu kwa aliyekuwa makamu wa Raisi Riek Machar kwa mazungumzo ya amani huko Addis Ababa nchini Ethiopia kuhusu mgogoro wa Sudan Kusini,Nayo serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo juma hili iliendelea kutangaza orodha mpya ya watu waliopewa msamaha kama ulivyotangazwa na raisi Joseph Kabila, Na kimataifa Israeli kujiondoa katika mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati, lakini pia hali ya usalama na ya kisiasa yaendelea kuwa mbaya nchini Ukraine.Ungana nami Reuben Kakule Lukumbuka kupata mengi zaidi yaliyojiri Wiki hii