KENYA-SOMALIA-Usalama

Takribani watu watatu wauawa katika mashambulizi mawili Mombasa Kenya

Usalama ukiimarishwa baada ya mkutokea milipuko mjini Mombasa
Usalama ukiimarishwa baada ya mkutokea milipuko mjini Mombasa www.telegraph.co.uk

Takribani watu watatu wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa jana Jumamosi katika mashambulizi mawili katika mji wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya, maafisa wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Mlipuko mmoja ulitokea katika eneo lenye pilika nyingi la Mwembe Tayari katikati ya mji, na lingine karibu hoteli maarufu ya Reef iliyoko ufukweni, katika eneo la Nyali.

Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya imethibitisha kuawa kwa watu hao watatu na karibu 15 kujeruhiwa huko Mwembe tayari baada ya guruneti moja au zaidi kurushwa ndani ya basi lililofurika abiria ambao walikuwa wamewasili punde kutoka mji mkuu Nairobi.

Wizara pia imesema kifaa hicho cha mlipuko au IED, kililipuka katika lango la Hoteli ya Reef, ingawa hakuna majeruhi walioripotiwa huku usimamizi wa hoteli ukisema wafanyakazi wake wote na wageni walikuwa salama.

Hakukuwa na madai ya haraka ya kundi lolote kuhusika na tukio hilo, ingawa mji huo umekuwa katika tahadhari ya uwezekano wa mashambulizi ya waasi wa Somalia wa kundi la Al Shabab au wanamgambo wa Kiislam wa nchini humo.

Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi tangu ipeleke jeshi lake kulinda amani nchini Somalia dhidi ya kundi la Al Shabab.