EU: kutokomeza ugaidi Afrika ya mashariki na kati
Wakati ukanda wa Afrika Mashariki na kati ukiendelea na juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi kwenye nchi zao, Umoja wa Ulaya unasema kuwa utashirikiana na nchi wanachama katika kuendesha operesheni maalumu kukabiliana na matukio haya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Kauli hii ya Umoja wa Ulaya inakuja wakati huu vyombo vya usalama nchini Kenya vikiendelea kukumbwa na sintofahamu kuhusu njia mbadala za kudhibiti mashambulizi ya kigaidi yanayotekelezwa na wapiganaji wa Al-Shabab toka nchini Somalia.
Balozi wa ujumbe wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Filberto Cerian Sebregondi kwenye mahoajino ya kipekee na rfikiswahili, amesema kuwa Umoja huo kwa kushirikiana na nchi wanachama wanaandaa mkakati wa kuanza kwa operesheni maalumu kukabiliana na ugaidi.
Balozi huyo amesema hayo baada ya watu watatu kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa juzi jumamosi katika mashambulizi mawili katika mji wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya.
Kenya imekua ikikumbwa wakati huu na mashambulizi ya mabomu na kusababisha vifo vya watu.