NIGERIA-CAMEROON-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria: Boko Haram yaapa kuwauza wasichana iliyowateka nyara

Sehemu ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria
Sehemu ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria Reuters

Wanafunzi waliotekwa nyara katikati ya mwezi wa aprili kaskazini mashariki mwa Nigeria watatumia kama “watumwa”, au “wauzwe” aidha “waolewe” kwa nguvu, ametangaza kiongozi wa kundi la Boko Haram katika mkanda wa video unaohifadhiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Matangazo ya kibiashara

“Nakiri kuwateka nyara wasichana ambao walikua ni wanafunzi. Nitawauza sokoni kwa jina la Allah”, amesema Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram, huku akibaini kwamba anawashikilia wasichana hao, ili nadharia na malezi kutoka mataifa ya kimagharibi viweze kusitishwa.

Kuna habari ambazo zimekua zikienea kote nchini kwamba wasichana hao watapelekwa nchini Chad na Cameroon na kuuzwa kwa bei ya dala 12 za kimarekani.

Wanamgambo wa kislamu wa kundi la Boko Haram, wakiwa na kiongozi wa kundi hilo Shekau Abubakar (katikati).
Wanamgambo wa kislamu wa kundi la Boko Haram, wakiwa na kiongozi wa kundi hilo Shekau Abubakar (katikati). AFP/File

Hayo yakijiri watu wawili, akiwemo askari polisi mmoja wameuawa nchini Cameroon katika shambulio liliyoendeshwa dhidi ya kambi moja ya polisi katika eneo la Kousseri kaskazini mwa taifa hilo, shambulio ambalo limedaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram, zimearifu duru za usalama.

“Wanamgambo wa kundi la Boko Haram wameshambulia usiku wa jana kuamkia leo kambi ya polisi. Wamemuua kwa risase mwenzetu (askari polisi) na raia mwengine ambae alikua amewekwa chini ya ulinzi, kimethibitisha chanzo cha usalama kilipohojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.

“Walikuja kumtafuta mmoja miongoni mwao ambae alikua anaziwiliwa katika kambi hio, na wamefaulu kumtorosha na wafungwa wengine amabao walukua wakiziwiliwa pamoja katika chumba kimoja, chanzo hicho kimefahamisha,bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

“Wakaazi wa mji waliamshwa kwa milio ya risase usiku wa jana. Asubuhi ndio tumepata taarifa kwamba wanamgambo wa kundi la Boko Haram wameshambulia kambi ya polisi, ameeleza kiongozi wa shirika moja la kihisani, Mey Ali.

Mkoa wa kusini mwa Cameroon, ambao unapakana na Nigeria, umekua ukikabiliwa na mashambulizi na mauwajiyanayotekelezwa na kundi la Boko Haram.

Mapadri wawili kutoka Itali na mtawa mmoja kutoka Canada walitekwa nyara mwanzoni mwa mwezi wa aprili katika mkoa huo, ambako familia moja ya raia kutoka Ufaransa walitekwa nyara na kundi hilo mwaka 2013.

Polisi na jeshi vikianzisha operesheni ili kutokomeza kundi la Boko Haram.
Polisi na jeshi vikianzisha operesheni ili kutokomeza kundi la Boko Haram. AFP PHOTO / Quentin Leboucher

Kundi la Boko Haram, ambalo lilitajwa na Marekani kwamba ni kundi la kigaidi, limekua likiendesha mashambulizi dhidi ya jeshi na kusababisha vifo vya raia wa kawaida tangu mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria. Jeshi la Nigeria lilianzisha hivi karibuni operesheni kabambe ili kujaribu kutokomeza kundi la Boko Haram.