AFRIKA KUSINI-Uchaguzi

Raia wa Afrika Kusini wanajianda kupiga kura

Kampeni ya mwisho ya chama cha ANC katika uwanja wa mpira wa Soweto, mei 4 mwaka 2014.
Kampeni ya mwisho ya chama cha ANC katika uwanja wa mpira wa Soweto, mei 4 mwaka 2014. RFI/Alexandra Brangeon

Wakati kampeni za urais nchini Afrika Kusini zikiwa zimetia nanga jana jumapili, chama tawala nchini cha ANC licha ya kukabiliwa na kashfa za matumizi mabaya ya ofisi bado kinatabiriwa kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi ulipangwa kufanyika jumatano ya wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama kipya cha Economic Freedom Fighters, Julius Malema.
Kiongozi wa chama kipya cha Economic Freedom Fighters, Julius Malema. REUTERS/Mujahid Safodien

Jana jumapili kiongozi wa chama kipya cha Economic Freedom Fighters, Julius Malema pamoja na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Democratic Alliance, Hellen Zille wamewataka wananchi kutumia kura yao kuleta mabadiliko nchini humo.

Hellen Zille ambaye chama chake kinapewa nafasi kubwa ya kutoa upinzani mkali kwa chama Tawala, amewaambia wananchi mjini Johanesburg ambako alihitimisha kampeni za chama chake, kwamba siku ya jumanne wasifanye makosa ya kuendelea kukiweka madarakani chama cha ANC.

Uchaguzi wa mwaka huu unatarajiwa kuwa wa aina yake kutokana na mvuto ambao vyama vya upinzani umekuwa nao, huku tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ikiahidi kuandaa uchaguzi ulio huru na haki.