MISRI-Siasa

Sisi: jeshi halitaingilia shughuli za uongozi wa nchi

Abdel Fattah al-Sissi  kiongozi wa zamani wa majeshi nchini Misri, ambae alitangaza hivi karibuni kwamba atagombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Misri.
Abdel Fattah al-Sissi kiongozi wa zamani wa majeshi nchini Misri, ambae alitangaza hivi karibuni kwamba atagombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Misri. REUTERS/Stringer

Aliyekuwa mkuu wa majeshi nchini Misri na kumuondoa madarakani rais Mohamed Morsi na baadaye kutangaza azma ya kugombea urais mkuu ujao nchini humo, Abdel Fattah al-Sisi ameahidi kuwa jeshi halitakuwa na mwanya wa kuingilia shuguli za uongozi wa nchi ikiwa atachaguliwa kuwa rais.

Matangazo ya kibiashara

Abdel Fattah al- Sisi ameyasema hayo jana katika mahojiano yake ya kwanza tangu atangaze kujiuzulu kuwa mkuu wa jeshi na yaliyotangazwa na vituo viwili binafsi vya televisheni zikiwa zinasalia siku ishirini tu kabla ya uchaguzi huo.

Aidha, Fattah al- Sisi amesisitiza kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais wa Misri, hatoruhusu vuguvugu la Muslim Brotherhood kuwa chama cha siasa.

Mapinduzi ya tarehe 3 mwezi julai mwaka uliopita yaliyoongozwa na Sisi yamefwatiwa na umwagaji damu pamoja na ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa Morsi ambao zaidi ya waandamanaji 1,400 wameuwawa ikiwa ni pamoja na zaidi ya 700 kwa siku moja mjini Cairo tarehe 14 mwezi Agosti mwaka 2013.

Wafuasi wa Mohamed Morsi, rais wa Misri aliepinduliwa madarakani na jeshi.
Wafuasi wa Mohamed Morsi, rais wa Misri aliepinduliwa madarakani na jeshi. AFP PHOTO/GIANLUIGI GUERCIA

Sissi anajiamini kwa umaarufu mkubwa alionao baada ya kumuondoa Morsi Madarakani na kuwakandamiza wafwasi wake jambo ambalo linamhakikishia ushindi katika uchaguzi wa tarehe 26 na 27 mwezi huu, hasa kwa vile hadi sasa hana mpinzani mwenye nguvu.