AFRIKA KUSINI

Matokeo ya uchaguzi mkuu yasubiriwa Afrika Kusini

Uchaguzi wa wabunge nchini Afrika Kusini umefanyika jana katika hali ya kuridhisha kwa mujibu wa waangalizi, huku matokeo ya awali yakisubiriwa kuanza kutangazwa hii leo majira ya asubuhi.

Zoezi la kuhesabu kura katika kituo cha kupigia kura cha Embo, magharibi mwa Durban, mei 7 mwaka 2014.
Zoezi la kuhesabu kura katika kituo cha kupigia kura cha Embo, magharibi mwa Durban, mei 7 mwaka 2014. REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ambao ni wa kwanza tangu kifo cha Nelson Madiba Mandela na wa tano tangu kuanguka kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994, umekamilika huku wapiga kura wakiripotiwa kujitokeza kwa wingi licha ya mawimbi ya kijamii ambayo yameitikisa nchi hiyo kwa miezi kadhaa.

Zoezi la uchaguzi mkuu katika mji wa Soweto nchini Afrika Kusini,Mei 7 mwaka 2014.
Zoezi la uchaguzi mkuu katika mji wa Soweto nchini Afrika Kusini,Mei 7 mwaka 2014. REUTERS/Mike Hutchings

Hamasa iliyoshuhudiwa jana katika uchaguzi huo inatafsiriwa na wachambuzi kuwa jibu la vijana wengi waliojitokeza hasa wale ambao ni mara yao ya kwanza kupiga kura na waliozaliwa baada ya mwaka 1994 ulioashuhudia mwisho wa utawala wa kipaguzi.

Matokeo ya awali yameanza kuwasili jana usiku katika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi mjini Pretoria kutoka vituo mbalimbali, lakini picha halisi ya matokeo hayo inatarajiwa kutangazwa Ijumaa jioni.

Ingawa serikali haikutangaza takwimu ya waliojitokeza, baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimezungumzia ushiriki wa zaidi ya ule wa mwaka 2009, tangazo lililofanana na lile la Tume ya Uchaguzi ambayo imezunguzia ushiriki mkubwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari saa nne kabla ya kufunga rasmi vituo kwenye majira ya saa tatu usiku.