DRC-Usalama

DRC: vurugu zasababisha vifo vya watu 15 katika uwanja wa mpira mjini Kinshasa

Kikosi cha wachezaji wa klabu ya TP Mazembe.
Kikosi cha wachezaji wa klabu ya TP Mazembe. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Idadi ya watu walipoteza maisha jana katika uwanja wa Tata Raphael jijini Kishasa wakati wa mechi baina ya Tout Poussant Mazembe na Vita Club imefikia watu takriban 15 na ewngine 21 wamejeruhiwa.

Matangazo ya kibiashara

“idadi imefikia kwa sasa 15 na wengine 21 wamejeruhiwa”, mkuu wa mkoa wa Kinshasa, Andre Kimbuta, ameambia vyombo vya habari.

Andre Kimbuta, amejielekeza pamoja na waziri wa mambo ya ndani, Richard Muyej, kwenye hospitali Mama Yemo, ambako miili 14 ya watu waliyopoteza maisha na majeruhi 11 waliyopelekwa.

Vurugu zilianza pale mashabiki wa clabu ya Vita Club waliposhindwa kuvumilia baada ya TP Mzembe kumiliki mchezo uwanjani katika kipindi cha kwanza na kuongoza kwa bao moja, wakati kipindi cha pili kikianza ndipo mashabiki wakaanza kurusha mawe uwanjani wakati mechi ikiendelea, jambo lililomlazimu Refa kusitisha mchezo.

Polisi ilitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya mashabiki wa klabu ya AS Vita Club, ambao walikua wakivurumisha mawe hovyo uwanjani.

Vurugu hizo zilisababisha kubomoka kwa ukuta wa uwanja na geti kung'olewa. Imethibitisha radio Okapi.

Habari zaidi zinaarifu kuwa msongamano wa mashabiki kuwania milango ya kuondoka uwanjani na hatuwa ya polisi kutumia bomu za kutowa machozi kuwatuliza mshabiki wa Vita Club ndivyo vilivyo sababisha mauaji hayo.

Mechi hiyo ilisitishwa katika dakika ya tatu ya kipindi cha pili cha mchezo ambapo Mazembe ilikuwa inaongza kwa bao moja kwa bila.

Mkuu wa mkoa wa Kinshasa amesema kwamba tume ya uchunguzi imeundwa ili kuchunguza waliyohusika na vurugu hizo, huku akibaini kwamba watakaopatikana na hatia wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.