Libya- Usalama

Libya yapoteza wanajeshi wanne

Hali ya usalama inaendelea kudorora katika mji wa Benghazi, nchini Libya.
Hali ya usalama inaendelea kudorora katika mji wa Benghazi, nchini Libya. © Mohammed Salem/Reuters

Wanajeshi wanne wa Libya wameuawa katika matukio mbalimbali mjini Benghazi mashariki mwa Libya, duru za hospitali na za usalamazimearifu

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wanne wameuawa na mwengine mmoja amejeruhiwa kwa risase ziliyopigwa na watu wasiyojulikana katika mji wa Benghazi, huku mwengine mmoja alijeruhiwa katika shambulio la kumuua liliyokua linamlenga”, mkuu wa kitengo cha usalama ameambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Msemaji wa Hospitali Al-Jala, Fadia Al-Barghathi, amethibitisha vifo vya wanajeshi hao.

Afisa mmoja wa ngazi ya juu jeshini ameuawa katika mtaa wa Al-Hadaek mjini kati, baada ya kushambuliwa kwa risase, lakini mwanae wa kiume ambaye walikua nae ndani ya gari ndogo alinusurika na shambulio hilo, amesema kiongozi mmoja wa jeshi.

Wakati huo huo, wanajeshi watatu wameuawa na mwengine mmoja amejeruhiwa katika mashambulizi tofauti katika mtaa wa Assalem, ameendelea kusema mkuu huyo.

Ramani ya Libya.
Ramani ya Libya. © RFI

Mji wa Benghazi umekua kwa sasa eneo la mashambulizi na mauaji yanayolenga jeshi na polisi. Mwezi desemba mwaka jana shambulio la kujitowa mhanga dhidi ya kituo cha polisi karibu na mji wa Benghazi ulisababisha vifo vya wanajeshi 13.

Hivi karibuni wanajeshi watano na askari polisi mmoja waliuawa na wengine 12 walijeruhiwa tarehe 2 mwezi mei mwaka huu katika makabiliano kati ya kikosi maalumu cha jeshi na makundi ya wanamgambo wa kislamu.

Wanamgambo hao wa kislamu wenye msimamo mkali wa kidini, ambao wana silaha nzito nzito wamekua wakinyooshewa kidole katika mashambulizi hayo, bila hata hivo kukiri iwapo wao ndio wanahusika.