Wahamiaji kutoka Afrika waendelea kukumbwa na ajali za majini
Takriban wahamiaji haramu 36 wamepoteza maisha na wengine 42 hawajulikani walipo baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya libya. Duru kutoka polisi nchini Libya zimearifu kuwa Boti hilo limezama kwenye umbali wa kilometa 4 katika pwani ya Garabuli, kilometa 50 mashariki mwa Libya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Watu 52 wameokolewa na miili 36 imeokotwa huku watu wengine 42 hawajulikani walipo, baada ya ajali hio.
Msemaji wa kikosi cha majiji Kanali Ayoub Kassem amesema wahamiaji hao ni kutoka katika mataifa mbalimbali barani Afrika akiwemo mama mjamzito miongozni mwa walipoteza maisha.
Kanali Ayoub Kassem ameongeza kuwa watu walionusurika katika ajali hio wamesema boti hilo lilikuwa limebabe watu 130 kutoka katika mataifa ya Mali, Sénégal, Gambia, Cameroun, Burkina Faso, na mataifa mengine barani Afrika.
Mkuu wa ujumbe wa shirikisho la kimataifa la wahamiaji (IOM), Othman Belbeisi, ameelezea masikitiko yake, kutokea kwa ajali hio, huku akitolea wito kwa mataifa husika kutafutia suluhu haraka iwezekanavyo ili kulinda maisha ya wahamiaji.
Kaimu waziri wa mambo ya ndani wa Libya, Salah Mazek, amesema Tripoli haiwezi kamwe kurahisishia wahamiaji kuingia kinyume cha sheria barani Ulaya, huku akiomba Umoja wa Ulaya kupatia ufumbuzi tatizo hlo.
Libya ni nchi, ambayo wahamiaji kutoka barani Afrika wamekua wakitumia kwa kuingia katika bara la Ulaya kwa kupitia katika bahari ya Mediterranean.
Maelfu ya raia wamekua wakifariki kila mwaka katika ajali kama hizo wanapojaribu kuingia Ulaya wanapotumia safari za majini.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, karibu wahamiaji 22.000 wakiwemo wakimbizi waliwasili katika pwani ya Italia wakitumia boti, wakati ambapo mwaka 2013 wahamiaji zaidi ya 220.000 walitumia usafiri wa majini kwa kuingia katika bara la Ulaya, hususan katika kisiwa cha Lampedusa.