UN-SUDANI KUSINI-Sheria

Ban Ki-Moon: uundwaji wa mahakama itakayo wahukumu wahusika wa mauaji Sudani Kusini

Ban Ki-moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akielezea hofu yake kuhusu mauaji yanayo endelea Sudani Kusini..
Ban Ki-moon, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akielezea hofu yake kuhusu mauaji yanayo endelea Sudani Kusini.. REUTERS/Andrew Burton/Pool

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amependekeza uundwaji wa mahakama maalum itayo wahukumu wahusika wa mauaji ya Sudani Kusini, kutokana na mapigano ambayo yanaendelea nchini humo, huku raia wakiendelea kupoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umaoja wa Mataifa, mjini New York.
Baraza la Usalama la Umaoja wa Mataifa, mjini New York. REUTERS/Eduardo Munoz

Akizungumza mbele ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban amesema kufuatia ripoti ya Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini, kuna haja ya kukiri kuwa mauaji ya kivita yametekelezwa nchini humo.

“Inafaa kufikiria kuunda mahakama maalum ya kimataifa kuhusu mauaji hayo”, amesema Ban.

Mahakama kama hizo, ziliundwa hususan kuhukumu wahusika wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Cambogdia na Yougoslavia ya zamani.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kikao hicho Ban Ki Moon amesema uundwaji wa mahakama hiyo ni jukumu la nchi wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Ban amesema, machafuko hayo yakiendelea idadi ya watu wanaopoteza maisha itaongezeka na raia wengi wataendelea kuyatoroka makaazi yao.

Akizungumza na vyombo vya habari, Ban Ki Moon amewatolea wito viongozi wanaohusika na mzozo huo, rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kuheshimu makubalinao waliofikia mwishoni mwa juma huko addis Ababa, Ethiopia.

Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) wakitia saini kwenye mkataba wa kusitisha mapigano, mjini Addis Ababa, ijuma mei 9 mwaka 2014.
Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) wakitia saini kwenye mkataba wa kusitisha mapigano, mjini Addis Ababa, ijuma mei 9 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametolea witio jumuiya ya kimataifa kuwajibika vilivyo ili kuhakikisha kuwa hali ya utulivu imerejea nchini Sudfani Kusini, huku akibaini kwamba bado kunahitajika dola za kimarekani milioni 781 ili ili kufikia kiwango cha dola za kimarekani bilioni 1.2 zitakazo tumiwa kwa misaada ya raia wa Sudani Kusini.