MAREKANI-CAR-Vikwazo

Marekani yawawekea vikwazo marais wa zamani wa CAR

Rais wa Marekani Barack Obama akizungumzia hali inayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Rais wa Marekani Barack Obama akizungumzia hali inayojiri nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. REUTERS/Junko Kimura-Matsumoto/Pool

Rais wa Marekani, Barack Obama ametangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao ni François Bozizé, Michel Djotodia pamoja na viongozi wengine wa tatu, ambao Marekani inawatuhumu kuchangia kwa vurugu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Dtotodia.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Michel Dtotodia. REUTERS/Herve Serefio

Amri hii , imekuja katika mfululizo wa vikwazo vilivyotangazwa Ijumaa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya watu watatu miongoni mwa viongozi wa hao watano, ili kuonyesha kuwa jumuiya ya kimataifa haitoendeleakuvumilia kauli za baadhi ya watu ambaazo zaonekana kuchochea chuki katika taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati. “Wale wanaohusika na vurugu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, watachukuliwa hatua za kisheria", amesema msemaji wa White House, Jay Carney.

Mbali na marais hao wa zamani Bozizé na Djotodia, amri ya Rais Obama inamhusu pia mratibu wa wa kundi la wanamgambo wa kikristo la Anti-balaka, Levy Yakété, pamoja na viongozi wawili wa kundi la zamani la waasi la Seleka, Nourredine Adam na Abdoulaye Miskine.

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé.
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozizé. REUTERS/Luc Gnago

Kulingana na amri hio, mali za viongozi hawa zitaziwiliwa nchini Marekani, na hawatoruhusiwa kukanyaga kwenye aridhi ya Marekani.

Obama pia ameamua kuanzisha mfumo wa vikwazo kwa pana zaidi , akibainisha kuwa hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ni "tishio (...) dhidi ya usalama na sera za kigeni zaa Marekani. "

" Tunaaomba pande zote kuacha ghasia , ili kuhakikisha kwamba sheria infuta mkondo wake na kwamba wale ambao wamejihusisha na ukiukwaji wa haki za binadamu wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria," Carney ameendelea kusema katika taarifa hio.

Hata hivo, "Sisi tumeshikamana na mataifa jasiri na tutaendelea kutolea wito raia ili wadumishe amani na maridhiano, " ameendelea kusema msemaji huyo, huku akibaini kwamba Marekani inaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa (...) na serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kuhakikisha kwamba taifa hilo limerejea katika hali yake ya usalama.