BURUNDI-APRODH-Sheria

Mwanaharakati wa haki za binadamu akamatwa Burundi

Kiongozi akiwa pia muasisi wa shirika la kutetea haki za binadamu na za wafungwa, Aprodh, Pierre Claver Mbonimpa amekamatwa mjini Bujumbua.
Kiongozi akiwa pia muasisi wa shirika la kutetea haki za binadamu na za wafungwa, Aprodh, Pierre Claver Mbonimpa amekamatwa mjini Bujumbua. Wikimedia

Kiongozi akiwa pia muasisi wa shirika la kutetea haki za binadamu na za wafungwa, Aprodh, Pierre Claver Mbonimpa amekamatwa jana usiku kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura, nchini Burundi alipokua akitaka kusafiri nchini Kenya na Kuwekwa jela.

Matangazo ya kibiashara

Mwanaharakati huyo amekua akifuatiliwa na viongozi wa Burundi na chama tawala CNDD-FDD, baada ya taasisi za Umoja wa Mataifa kuitolea onyo kali serikali ya Burundi zikiituhumu kuwapa silaha vijana wa chama tawala CNDD-FDD.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi wamelani kukamatwa kwa mwenzao na kusema kwamba hawatositisha harakati zao kutokana na vitisho vinavyoendesha dhidi yao.

Kiongozi huyo wa shirika la Aprodh amekamatwa na afisa wa idara ya upelelezi ambae anajulikana kwa jina la Ichard, ambae amemuonyesha mwanaharakati huyo hati ya kumkamata iliyotolewa na muendesha mashitaka katika manispa ya jiji la Bujumbura.

Pacifique Nininahazwe,kiongozi wa muungano wa vyama vya kiraia Focode.
Pacifique Nininahazwe,kiongozi wa muungano wa vyama vya kiraia Focode. AFP PHOTO/ROBERTO SCHMIDT

Kiongozi wa muungano wa vyama vya kiraia, Focode, Pacifique Nininahazwe, amesema kushangazwa na kukamatwa kwa Pierre Claver Mbonimpa, wakati alikua na waranti wa kuripoti mahakamani jumatatu Mei 19.

Wakili wa mwanaharakati huyo, Armel Niyongere, ameelezea kitendo cha kukamatwa mteja wake kama ukiukwaji wa haki za binadamu.