KENYA-Usalama

Zaidi ya watu 10 wauawa na 70 kujeruhiwa katika shambulizi Nairobi

Mmoja wa raia akipita kando ya basi dogo la abiria ambalo lilishambuliwa hii leo kwenye soko la Gikomba jijini Nairobi
Mmoja wa raia akipita kando ya basi dogo la abiria ambalo lilishambuliwa hii leo kwenye soko la Gikomba jijini Nairobi RFI

Watuhumiwa wawili wa ugaidi wanashikiliwa na jeshi la kenya baada ya Milipuko miwili kutekelezwa jana jijini Nairobi katika soko la gikomba na kusababisha vifo zaidi ya kumi na majeruhi 78.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linajiri wakati huu hofu ikitanda katika jamii ya kimataifa ambapo Uingereza imewaondosha watalii raia wake mia 6 na kuahirisha mara moja ziara za kitalii nchini Kenya.

Mamlaka nya utalii nchini Kenya imekadiria hasara baada ya kuahirishwa kwa ziara za kitalii nchini humo kufikia takribani bilioni 5 na kuilaumu serikali ya kenya kwa kushindwa kuchukua hatua za mara moja kukomesha vitendo vya kigaidi.

Naye Raisi Uhuru Kenyatta, ambaye alizungumza muda mfupi baada ya mashambulizi hayo alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kushirikiana na kenya kukabiliana na ugaidi ambao unakua kwa kasi na kutatiza ulimwengu mzima.

Katika hatua nyingine marekani imelaani mashambulizi yaliyotekelezwa jijini Nairobi na kuita ni ya woga kwa vile yamelenga raia wasiokuwa na hatia na kuahidi kushirikiana na kenya kuutokomeza ugaidi.