MALAWI-Siasa-Uchaguzi

Wananchi wa Malawi wachagua viongozi wapya

Wanachi wa nchi ya Malawi wanapiga leo kura kumchagua rais, wabunge na madiwani ambapo wagombea urais kumi na wawili wako mbioni akiwemo rais Joyce Banda ambaye yuko madarakani kwa muda wa miaka miwili tu baada ya kifo cha hayati rais Bingu wa Mutharika.

Wananchi wa Malawi wakipiga kura
Wananchi wa Malawi wakipiga kura Nyasa Times
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya vijana hamsini wameandamana kwa kushitukiza mapema leo asubuhi, wakiimba nyimbo zinazoikashifu serikali.

“Serikali imeanda vibaya uchaguzi, ikiwa na lengo la kuiba kura”, amsema Paul Wind, kijana mwenye umri wa miaka 38, huku akibaini kwamba wakiwazuia kuchagua wa takaua wamekosea.

Wagombea ni kumi na mbili. Rais anaeondoka madarakani Joyce Banda, mwenye umri wa miaka 64 iko madarakani kwa muda sasa wa miaka miwili. Hata hivo rais huyo aliengia madarakani bila kuchaguliwa, baada ya kifo cha aliekua rais wa Malawi Bingu wa Mutharika, anafanya kila kiko chini ya uwezo wake ili ashinde uchaguzi huo, licha ya kuwa taifa hilo linakabiliwa na mdororo wa kiuchumi, wakati serikali yake iimekua ikikabiliwa pia na kashfa ya ufisadi.

Joyce Banda amewahi kusema kwamba ufisadi huo uligunduliwa baada ya yeye mwenyewe kuanzisha zoezi la kukabiliana na rushwa, huku akikanusha kutohusika na kashafa hio.
Mpinzani wake mkuu ni waziri wa zamani wa mambo ya kigeni Peter Mutharika, mwenye umri wa miaka 74, ambaye ni ndugu wahayati rais Bingu wa Mutharika.

Mgombea mwengine ambae anaonekana kuleta upinzani mkali katika kinyang'aniro hicho ni mwanae rais wa zamani Bakili Muluzi, Atupele Muluzi, mwenye umri wa miaka 36, pamoja na Lazarus Chakwera, mwenye umri wa miaka 59, kutoka chama cha hayati rais Kamuzu Banda ambacho hakipo madarakani kwa miaka 20 sasa.

Kwa mara ya kwanza, uchaguzi huo unagubikwa na ushindani mkubwa baina ya wagombea.

Vituo vya kupigia kura 4,475 vimefunguliwa tangu saa 12 asubuhi na vitafundwa saa12 jioni.

Uchaguzi huu ambao ulitanguliwa na kampeni za vyama vya kisiasa ambazo ziliendeshwa kwa utulivu, hata kama kuna vifo vya watu watatu viliyotokea katikati mwa mwezi wa Machi katika kampeni ya rais anaeondoka madarakani Joyce Banda katika ngome ya mpinzani wake mkuu Peter Mutharika.

Kutakuweko na duru moja katika uchaguzi huo, na matokeo yanasubiriwa mnamo siku 8.

Huu ni uchaguzi wa tano tangu mwaka 1994, baada ya kuweko na mfumo wa vyama vingi nchini Malawi. Wapiga kura watawachagua pia madiwani 462.