DRC-UFARANSA-CAR-Diplomasia

DRC: Joseph Kabila ziarani Ufaransa

François Hollande na Joseph Kabila mjini Kinshasa, le Oktoba 13 mwaka 2012.
François Hollande na Joseph Kabila mjini Kinshasa, le Oktoba 13 mwaka 2012. REUTERS/Noor Khamis

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila anakutana leo alaasiri mjini Paris na mwenyeji wake, François Hollande, katika kikao kiliyoandaliwa kuhusu mzozo unaoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya Jamhuri ya kidemokrasia na Ufaransa yanashiriki kwa pamoja katika mpango kusaka amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina wanajeshi 850 na askari polisi 150 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao walitumwa kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika ili kusimamia amani nchini humo.

Baadhi ya mashirika ya kiraia yalikosoa vikali kutumwa kwa wanajeshi hao nchini jamhuri ya Afrika ya Kati wakati serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikipambana na zaidi ya makundi 40 ya watu wenye silaha mashariki mwa Congo, huku hali ya usalama ikiendelea kudorora

Miezi 5 tangu wanajeshi wa Congo kuwasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameanza sasa kufanya vizuri licha ya changamoto nyingi kuwakabili, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa wanajeshi wawili mjini Bangui.

Ufaransa na uongozi wa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanapongeza sana umahiri wa wanajeshi wa Congo katika operesheni wanazoendesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ufaransa imeitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kubakiza wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati mataifa mengi barani Afrika yamependekeza kutuma wanajeshi wao nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mfano kama Afrika Kudsini, huku mataifa mengine yakihofia kutuma wanajeshi wao, na Chad tayari imewaondoa wanajeshi wake yapata sasa mwezi moja.

Huenda Ufaransa ukaiomba Jamhuri ya Kidemokrasia kuongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wanajeshi wa DRC (FARDC).
Wanajeshi wa DRC (FARDC). AFP PHOTO/STRINGER

Kwa upande wa serikali ya Congo, inabaini kwamba mzozo unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo una taswira ya kimataifa, na ni fursa kwao kuonyesha umahiri wa wanajeshi wake katika kanda ya Afrika ya kati, lakini pia kuzuia kabla machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya yasivuke mpaka na kuingia nchini Congo.