MISRI-Usalama

Misri: shambulio la bomu lawajeruhi askari polisi katika jimbo la Sinaï

Watu wengi waliangamia katika mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Sinaï.
Watu wengi waliangamia katika mashambulizi yaliyotokea katika mji wa Sinaï. REUTERS/ Stringer

Wanajeshi saba na raia wawili wa kawaida wamejeruhiwa usiku wa jana katika mlipuko wa bomu uliyotokea katika mji wa Al-Arish, katika jimbo la Sinaï, duru za usalama zimefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilikua limelenga kifaru cha polisi katikati ya mji wa Al-Arish, wamesema viongo tawala wa mji huo.

Baada ya mlipuko huo, kulisikika milio ya risase kati ya kikosi cha usalama na watu wanaoshukiwa kuendesha shambulio hilo, ambao walifaulu kutimka.

Polisi na jeshi vimekua vikilengwa nchini Misri katika mfululizo wa mashambulizi yanayoendeshwa na makundi ya wanamgambo wa kislamu, wakibaini kwamba ni ulipizaji kisase dhidi ya mauaji ya wafuasi wa rais, Mohamed Morsi, aliyeng'atuliwa madarakani na jeshi, Julai 3 mwaka 2013.

Polisi ikwakamata wafuasi wa vuguvugu la Muslim brohterhood, katikamaandamano ya kumuunga mkono rais Mohamed Morsi alieng'atuliwa madarakani.
Polisi ikwakamata wafuasi wa vuguvugu la Muslim brohterhood, katikamaandamano ya kumuunga mkono rais Mohamed Morsi alieng'atuliwa madarakani. AFP Photo/STR

Mengi ya mashambulizi hayo yaliendeshwa katika jimbo la Sinaï, ngome kuu ya wapiganaji wa kiislamu, huku miji ya Cairo na Nil Delta yakikumbwa na mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu wengi.

Mashambulizi hayo yaliyoanzishwa tangu mwezi Julai mwaka 2013 yamesababisha vifo vya wanajeshi na askari polisi 500, kulingana na taarifa iliyotolewa na serikali ya mpito iliyoundwa na kuongozwa na jeshi tangu alipoondolewa madarakani Mohamed Morsi.